Habari za Punde

Taarifa Ya Serekali Kuhusiana na Uvumi Uliosambazwa kwa Wananchi Kuhusiana na Mwalim Haroun Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ametowa Taarifa ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusiana na Uvumi ulioenezwa na baadhi ya Wananchi wa Mji wa Zanzibar kuhusianana kufariki kwa Mhe. Mwalim Haroun Suleiman,  kuwa si za kweli na anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Nchini Afrika kusini.

Balozi Seif  amesema hali ya  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini na anaendelea na matibabu yake katika hospital hiyo akiwa chini ya uangalizi wa daktari wake anayemshughulikia.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akitowa taarifa hiyo maalum ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wananchi wa Zanzibar kukanisha uvumi huo ulioenezwa na Watu wasiojulikana kupitia njia ya mitandao na kuusambaza sehemu mbalimbali za Zanzibar na Vitongoji vyake.

Amesema Mhe. Haroun ameaza kuumnamo januari 5, mwaka huu na kufanyiwa vipomo katika Hospitali ya Mnazi mmoja na kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi na baadae kusafirika Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu zaidi ya Afya yake kufanyiwa uchunguzi.


Balozi Seif amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini na Mtoto wake  Mhe. Maalim Haroun amesema Baba yake amefanyiwa upasuaji januari 24, na hadi sasa hali yake ya afya inaendelea vizuri na anaendelea na kufanya mazoezi.

Balozi Seif amewata Wananchi kutambua ukweli huo na kuachana na uvumi usio na ukweli kwa kiongozi huyo.

Mhe Maalim Haroun yuko mzima wa afya na anaendele na matibabu yake katika moja ya hospital nchini afrika kusini.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.