Na
Khamisuu Abdalla
KUWEPO
idadi kubwa ya wazazi wanaozalia wodini katika hospitali kuu ya Mnazimmoja, linatokana
na ongezeko la wajawazito katika hospitali hiyo.
Muuguzi
dhamana wa wodi ya wazazi wa hospitali hiyo, Tatu Fundi Salum, alisema kuanzia
mwezi Januari hospitali hiyo inazalisha kati ya wajawazito 70 hadi 89 kwa siku.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mnazimmoja,muuguzi huyo alisema
upungufu wa vitanda katika chumba maalum cha kuzalia ndio chanzo,
kilichosababisha wajawazito kujifungulia wodini.
Aidha
alisema kutokana na ongezeko la wazazi, kitanda kimoja kinatumiwa na wajawazito
hadi watatu kwa wakati mmoja huku wodi nzima ikiwa na vitanda 47 pekee.
"Chumba
cha kuzalisha (‘leba’) kina vitanda vitatu tu na kama unavyoona kwa siku
tunazalisha watu wengi, leba kunajaa na kama mzazi yuko tayari kujifungua,
tunalazimika kumzalisha palepale wodini,” alisema.
Alisema
kufurika wajawazito katika hospitali hiyo kunatokana na wazazi kupuuza
utaratibu uliowekwa wa kuzitumia hospitali nyengine kwa ajili ya
kujifungua,ikiwemo hospitali za Muembeladu na Mpendae.
"Wodi
ya wazazi sasa kama tumo sokoni wajawazito wengi sana na vitanda vyetu ni 47 tu
havitoshelezi kwa wajawazito wote, sasa hutulazimu kuwaweka wajawazito hadi
watatu katika kitanda kimoja,” alisema.
Alisema
mzazi anapojifungua salama huwekwa kwa saa 6 kumchunguza zaidi huku wajawazito
wanaozaa kwa upasuaji huwaweka kwa siku tatu.
Alisema
kwa kawaida mzazi anapojifungua hutakiwa kubakia hospitali kwa saa 24 na
wanaofanyiwa upasuaji hutakiwa kukaa siku tano.
Hata
hivyo, alisema kiutararibu wazazi wanapojifungua mtoto wa pili hawatakiwi
kwenda hospitalini hapo ikiwa watakua hahana matatizo, lakini wazazi wanakuwa
wakaidi na hata ukiwarejesha waende hospitali nyengine huwa hawakubali.
Alisema
kutokana na tatizo hilo, walipeleka maombi hopsitali ya KMKM Kibweni kupatiwa
nafasi kwa ajili ya wajawazito na kukubaliwa lakini changamoto kubwa ni ukosefu
wa vifaa vya kuzalisha.
Hivyo
aliiomba serikali kuwatafutia sehemu mbadala ya kuwajenga wodi ya wazazi kwa
sababu hospitali ya Mnazimmoja haitoshelezi.
Pia
aliwaomba wazazi waliowahi kujifungua katika hospitali hiyo, wazitumie
hospitali nyengine za serikali ili kupunguza msongamano.
Wazazi
9 walipoteza maisha kwa kipindi cha Januari hadi Machi kutokana na kifafa cha
mimba na kupoteza damu nyingi.
0 Comments