Habari za Punde

DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NCHI ZA NJE WA UTURUKI.

- Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo, Mei 30, 2014.  Katika mazungumzo yao walisisitiza juu ya ushirikiano katika Nyanja mbalimbali baina nchi hizi mbili .  Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014. Picha na OMR


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.