WAANDISHI wa habari wengi wamekuwa wavivu
wa kuandika habari za vijijini, na kuandika zaidi habari za misafara ya viongozi
na semina, ambapo pichani waandishi wa habari, kushoto wakioongozwa na
mwandishi wa kujitegemea, Omar Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa jumuia ya ‘JAMBO
GROUP’ ya Kwazani Wambaa Mkoani, wakiwa na zawadi za matunda, baada ya
kuwafikia na kuawandikia habari (picha
na Haji Nassor, Pemba)
WAPIGANAJI wa Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba,
wakimsikiliza Afisa mpiango wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la
Pemba Khalifan Amour hayupo pichani, alipokuwa akizungumza nao, kujua mafanikio
na changamoto zinazowakabili, ambapo ujumbe wa ZSLC hujiwekea utaratibu wa kutembelea
vyombo vinavyosimamia sheria kila mwaka (picha
na Haji Nassor, Pemba)
MKUU wa wilaya ya Wete Pemba, Omar Khamis Othuman,
akifungua mdahalo wa wazi kwa wanajumuia za kiraia, ili kujenga mbinu ya
kushirikiana na kamati za kudumu za baraza la wawakilishi, katika kujadili na
kutoa michango yao katika miswada ya sheria, kulia ni Mwenyekiti wa PACSO Omar
Ali Omar na kushoto ni mfafanuzi wa mada, Juma Bakari Alawi, mdahalo huo uliofanyika
skuli ya sekondari ya Fidel castro (picha
na Haji Nassor, Pemba)
WANAFUNZI wanaokaa skuli ya
sekondari ys Fidel castro Pemba, wakiwa katika harakati za kugawana mlo wa
mchana skulini hapo, baada ya kukabidhi beseni ya chakula na muhusika wa chakula
na kisha kujigawawiya wenyewe (piccha na
Haji Nassor, Pemba)
MWALIMU Mkuu skuli ya maandalizi ya ‘STAR’ iliopo
Kichungwani wilaya ya Chakechake Pemba, Moza Said Salum akimkabidhi mwanafunzi
wake, ambae ni mshindi wa mchezo wa kuokota mbatata, uliofanyika ili kuwaaga
wenzao waliomaliza elimu ya maandalizi, sherehe hizo zilifanyika uwanja wa
tenis Chakechake (picha na Haji Nassor,
Pemba)
No comments:
Post a Comment