Ndugu zangu hawa watu wa shirika la Umeme wako wapi inafikia waya wa umeme kupita juu ya paa la nyumba na kuwekewa tambara kuzuiya kuchunika, hii ni hatari kwa wananchi wanaokaa katika nyumba hii huko kinuni siku waya huo ukiwa tayari umeshachunika na kuleta madhara kwa wananchi wa nyumba hii nani wa kulaumiwa ? ZECO au Mwananchi huyu . jioneeni wenyewe na kutowa maamuzi ya jambo hili kazi kwenu wahusika. Kadhia hii imeiona wakati nikiwa katika tembea yangu kinuni leo asubuhi.
Kasharunga FC Yatwaa Ubingwa wa Mia Mia Cup Msimu wa 9
-
Na Diana Byera,Muleba
Timu ya Kasharunga FC imetwaa ubingwa na kujishindia kitita cha Shilingi
Milioni 10 baada ya kuifunga Muhalila Cup All Starts kwa mi...
3 hours ago
Inasikitisha, kwa Zeco inaonesha haya ni ya kawaida kwao. Yapo maeneo mengi mfano Wa haya. Ukienda pale Mwembe mchomeke kwenye mashine za maji kuna waya ziko chini kabisa name watoto wanacheza Mpira hapohapo. Mola atustiri
ReplyDelete