Habari za Punde

Zanlink Yasimamia Mafunzo ya Cyberoam kwa Maofisa wa IT Zanzibar.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zanlink Ndg Sanjay Raja, akifungua mafunzo ya Kimataifa ya Cyberoam kwa maofisa wa IT wa Wizara za Serikali na Makampuni ya Binafsi, jinsi ya matumizi ya Mawasiliano kupitia mitandao, Mafunzo hayo yamewashirikisha Vijana 18 kutoka sekta mbalimbali za Serikali na Binafsi yatakuwa kwa muda wa siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zanlink, akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree Shangani Zanzibar.
Washirikiwa wa mafunzo hayo yakifuatilia ufunguzi wake katika ukumbi wa hoteli ya Double Tree shangani Zanzibar.
Muwezeshaji wa mafunzo hayo ya Cyberoam, Ndg. Samson Ogada, akitowa mada katika mafunzo hayo makubwa yalioandaliwa na Zanlink Zanzibar kwa Maofisa wa Wizara za Serikali na Kampuni Binafi kupata elimu ya matumizi mazuri ya mitandao, yaliowashirikisha jumla ya Vijana 18 wanapata mafunzo hayo kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa hoteli ya double tree shangani Zanzibar. 
Muwezeshaji wa mafunzo hayo ya Cyberoam, Ndg. Samson Ogada,akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo akiwasilisha mada. kuhusiano na matumizi ya mitandao.  

     washiriki wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini kupata utaalim kupitia mafunzo hayo ya Cyberoam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.