Habari za Punde

Kamati Kuu ya CCM Yakutana Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Dk. Jakaya Kikwete.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, (katikati) Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana.alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM uliofanyika Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake DK Jakaya Mrisho Kikwete.    
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduz, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria Kikao cha Kawaida cha Kamati Kuu ya CCM, akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abrahamani Kinana 
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kisiwandui kuhudhuria Kikao cha Kamati Kuu ya CCM.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya CCM.kilichofanyika Zanzibar Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.

WAJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, wakimsikiliza Mhe Salim Ahmeid Salim akizungumza na Mhe Shamsi Vuai Nahodha na kulia Mhe Samia Suluhu Hassan, wakibadilishana mawazo kabla ya kuaza kwa kikao hicho kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Wajumbe wa mkutano wa Kamati Kuu ya CCM wakipitia makabrasha yao kabla ya kuazi Kikao hicho cha siku moja kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibarm


Wajumbe wakipitia Makabrasha yao kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliofanya Kikao chake cha siku moja Zanzibar.
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa katika chumba cha mkutano wakibadilishana mawazo wakisubiri kufunguliwa kwa mkutano huo na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Jakaya Kikwete, ikiwa Kikao cha Kawaida.
VIONGOZI wa CCM meza kuu wakipiga makofi baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mkutano Afisi Kuu ya CCM Zanzibar,kutoka kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu Mkuu wa CCM Ndg, Abrahaman Kinana na Makamu Mwenyeki wa CCM Bara Ndg Philip Mangura.
KATIBU Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana, akitowa maelezo ya Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. jakaya Kikwete akifungua Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM kisiwandui kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk, Ali Mohamed Shein,

WAJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Taifa akifungua Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kikiwa kikao cha kawaida kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.