Kutokana na utafiti
mpya, zaidi ya watu bilioni moja watakabiliana na maisha ya umaskini
uliokithiri kama viongozi hawatafanya maamuzi muhimu juu ya umaskini, kukosekana
kwa usawa na mabadiliko ya hali ya hewa katika mikutano miwili muhimu ya New
York na Paris baadaye mwakani.
Hiyo ni tahadhari iliyotolewa na zaidi ya
taasisi elfu moja dunia nzima ambazo zimeungana kuzindua kampeni inayoitwa
hatua/2015, zikiwataka viongozi wa kitaifa na dunia kuchukua hatua za haraka na
madhubuti ili kuondoa mabadiliko ya hali ya hewa yanayosabishwa na shughuli za
binadamu, kumaliza umaskini na kushughulikia swala la matabaka.
Mahesabu mapya yaliyotolewa na hatua/2015 yanaonyesha
idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri-chini ya shilingi elfu
mbili kwa siku-inaweza ikapunguzwa kutoka zaidi ya bilioni moja hadi milioni
360 ifikapo mwaka 2030.
Hata hivyo, kama
viongozi watashindwa kuendeleza kasi iliyopo ya mikakati ya maendeleo kwenye Mkutano Maalumu
wa Umoja wa Mataifa juu ya maendeleo endelevu mwezi wa tisa na Mkutano wa Umoja
wa Mataifa kuhusu mazingira mwezi wa kumi na mbili, na wakapunguza juhudi zao,
watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri wataongezeka hadi kufikia bilioni
moja na laki mbili ifikapo mwaka 2030. Ongezeko hili litakuwa la kwanza kwa
kizazi hiki toka mwaka 1993 na ni zaidi ya ongezeko la watu bilioni moja
(milioni mia nane sitini na sita) ukilinganisha na kama hatua stahiki
zingechukuliwa. Kwa hali hii, mmoja kati ya kila watu watatu duniani ataishi
chini ya shilingi 2500 kwa siku.
Malala Yousafzai, mshindi
wa tuzo ya Nobel ambaye aliweka maisha yake hatarini kwa sababu ya elimu
anasema;
“Mwaka 2015 ni lazima
uwe mwaka wa dunia kuamka na kuhakikisha dunia salama na yenye haki kwa watoto
na vijana. Wote lazima tupambane kuhakikisha hili linatokea. Usipoteze nafasi
hii’’
Pamoja na Malala,
watu wengine wanaharakati mashuhuri wakijumuisha Askofu Desmond Tutu, Mo
Ibrahim, Angelique Kidjo, D’banj, Malkia Rania wa Jordan, Bono, Ben Affleck,
Bill na Melinda Gates na Ted Turner wanaunga mkono muunganiko wa taasisi zaidi
ya elfu moja kwnye nchi zaidi ya 120 duniani. Kampeni inatoa wito kwa viongozi
wa dunia kukubaliana juu ya mipango ya ya kumaliza umaskini, kuzuia madadiliko
ya hali ya hewa na kukabiliana na ukosefu wa usawa.
Hatua/2015 ambayo ilitangazwa na Malala
wakati akipokea tuzo ya Nobel-ni moja kati ya kampeni kubwa zaidi zilizowahi
kuanzishwa ikijumuisha mazingira, haki za binadamu, taasisi za maendeleo na
jumuia za kidini. Kutoka kwenye makampuni maarufu kama Amnesty International na
Save the Children, hadi taasisi za kampeni na utetezi kama ONE, hadi taasisi
zinazofanya kazi na jamii, harakati hizi zinadhamiria kuhakikisha makubaliano
ya mwaka 2015 yanaundwa na watu.
Kwa Tanzania, vijana
wamekutana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dr Mohamed Gharib Bilal kwa majadiliano
juu ya matarajio yao kwa ajili ya baadaye na hatua wanazotaka viongozi wao wa
kisiasa wazichukue mwaka 2015.
Mmoja wa vijana hao,
Eva, ambaye na miaka 14 anasema;
“Mwaka huu
ninapotimiza miaka 15, viongozi watakubaliana juu ya mpango wa kuifanya dunia
iwe bora zaidi. Kama wakifanikiwa kuifanya vizuri, na wakaisimamia, kwa hakika
hapatakuwa na watu wenye umaskini uliokithiri popote duniani wakati ntakapokuwa
nafikisha miaka 30. Ni maisha yetu ya baadaye yaliyo kwenye hati hati. Ndio maana
mimi na maelfu wenzangu tunataka viongozi wetu wafanye maamuzi sahihi ifikapo
mwaka 2015’’
Dr Sipho S. Moyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa ONE Afrika anasema;
“Dira ya maendeleo ya
Tanzania ya mwaka 2025 ni kuitoa nchi kutoka kipato cha chini hadi kipato cha
kati ifikapo mwaka 2015. Kwa hili kufanikiwa, sera sahihi zenye vipaumbele
lazima ziwekwe ili kukabiliana na umaskini uliokithiri na kukosekana kwa usawa
kwa kutoa fursa za kijamii kama elimu bora na kuwezesha mazingira ambayo
Shirika la Kazi la Kimatifa linaita ajira yenye staha. Ni muhimu kwa hiyo
serikali iende kwa kasi na kiufanisi katika kutekeleza mkakati wake wa Matokeo Makubwa Sasa, ambao unalenga katika kuongeza msisitizo na dhamira
ya serikali katika kuondoa umaskini na njaa na hivyo kuufanya mwaka 2015 kuwa
mwaka utakaoleta nchi hii karibu na mafaniko makubwa kwa kila mtu hapo baadaye’
Margaret
Mliwa – Mkurugenzi Mkazi wa Restless Development anasema:
‘Uzinduzi wa
hatua/2015 ni muhimu kwa vijana wa Tanzania, kwani unafungua njia ya
majadiliano baina ya vijana na viongozi wao. Kwa hatua na juhudi za pamoja za
kushinikiza maamuzi muhimu kwa mwaka 2015 ili kukabiliana na umaskini na
ukosefu wa usawa, sote tunaweza kuifanya Tanzania mahali bora zaidi’
Kwa upekee
kabisa, kwa hakika huu ni mwaka wa vijana wa Tanzania kuhamasika na kuhakikisha
maamuzi yatakayofanywa na serikali yao yanawakilisha aina ya Tanzania
wanayotaka kuiona.
Kama sehemu ya
uzinduzi wa kampeni ya hatua/2015, shughuli tofauti zinaendelea kwenye zaidi ya nchi 50
duniani. Nyingi zinaongozwa na watoto wenye miaka 15-ambayo ndio sehemu kubwa
ya watakaothirika na makubalino ya mwaka huu.
·
Nchini Uganda, vijana watazungumza na
Waziri wa Mambo ya Nje kumtaka asikilize matakwa yao wakati wakimkabidhi mswada
uliosainiwa na zaidi ya vijana 10,000
·
Nchini Nigeria, watoto wa miaka 15
watamuuliza maswali waziri wa fedha, Ngozi Okonjo-Iweala kwenye televisheni ya
taifa
·
Nchni Afrika Kusini, vijana wa miaka kumi
na tano kutoka nchi nzima watakutana na waziri wa Michezo, Fikile Mbalula
katika mji wa kihistoria wa Soweto kumtaka ajiunge nao katika kuwaandalia
mazingira salama kwa ajili ya kizazi chao.
·
Jijini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki- moon atakutana na
kundi la vijana wa miaka 15 kujadili kwanini wanahitaji dunia ichukue hatua
mwaka 2015
·
Nchini Uingereza, baadhi ya wanaharakati vijana
watakutana na Waziri Mkuu David Cameron na Ed Miliband, kiongozi wa Upinzani,
kuwataka kuchukua fursa iliyopo mwaka 2015.
Hatua/2015 inatoa wito kwa wananchi kujiunga nao kuhakikisha viongozi wa
dunia wanajikita kuboresha dunia. Mwaka 2015 kampeni itatoa fursa kwa yoyote na
popote alipo kushiriki katika kushawishi matokeo ya majadiliano haya ya dunia
ili kuweza:
•
Kumaliza umaskini wa
aina azote
•
Kupata haki za watu
za msingi, kumaliza matabaka na ubaguzi
•
Dunia ambayo yeyote
anaweza kushiriki na kuwawajibisha viongozi wake
0 Comments