Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati (katikati) Mh: Ramadhan Abdallah Shaaban akitoa shukran zake mbele ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Mazingira kutoka Norway wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe huo katika ukumbi wa Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati (AMMN) Forodhani Zanzibar.
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Waziri wa Ardhi
Makaazi Maji na Nishati, Mh: Ramadhan Abdallah Shaaban (hayupo pichani) katika
mkutano wa pamoja na Kamati ya Nishati na Mazingira kutoka Norway ujumbe
uliofika Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati (AMMN) na kufanya mazungumzo
na watendaji wa Wizara pamoja na ZECO.
Baadhi wa wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano huo
Katibu Mkuu Wizara ya AMMN, Ali Khalil Mirza (wa pili
toka kushoto) akielezea jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Mazingira ya
Bunge la Norway. Ujumbe huo umefika nchini kwa lengo la kuangalia utekelezaji
wa miradi mbali mbali inayofadhiliwa kupitia Shirika la Maendeleo la Norway
(NORAD)
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO),
Mhandisi: Hassan Ali Mbarouk akiwasilisha mada mbele ya ujumbe kutoka Norway
juu ya mafanikio ya utekelezaji wa awamu nne za mradi wa usambazi umeme
vijijini uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Nchi ya Norway (NORAD) katika
ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati (AMMN) Forodhani
Zanzibar.
(Wa kwanza kushoto) Waziri wa AMMN, Mh: Ramadhan
Abdallah Shaaban akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya AMMN, Ali Khalil Mirza na
Wajumbe kutoka nchi ya Norway wakifuatilia muwasilisho unaotolewa na Meneja
Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk (hayupo pichani)
juu ya mafanikio ya utekelezaji wa awamu nne za miradi ya usambazaji umeme
vijijini.
Mjumbe kutoka Bunge la nchi ya Norway akiuliza suala
kwa muwasilishaji wa mada ambae ni Meneja Mkuu wa ZECO, Hassan Ali Mbarouk
(hayupo pichani) juu ya ripoti ya utekelezaji wa miradi iliyosimamiwa na nchi
hiyo.
Baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya AMMN na Shirika
la Umeme (ZECO) wakifuatilia mkutano huo
Ujumbe kutoka nchi ya Norway ulitembelea na kuona baadhi ya kazi za ujasiriamali zinazotumia umeme ambapo walitembelea kiwanda cha kupasua na kusafisha mbao kilichopo Mkwajuni Kaskazini Unguja na Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni na kuona jinsi umeme unavyotumika katika shughuli hizo
Wawaeleze pia muda gani wanachukua kumpatia umeme mteja tokea tarehe anapotuma maombi. Na kwa Nini hawako aggressive kupeleka miundombinu ya umeme maeneo ya makaazi mapya.
ReplyDelete