WANAFUNZI wanaohitimu masomo mbali mbali katika Chuo
cha Zanzibar College of Business Education (Z.C.B.E)Kisiwani Pemba, wakiwa
katika maandamano ya kuingia katika eneo la mahafali yao, ambapo Makamo wa Pili
wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi alikuwa mgenirasmi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe: Balozi Seif
Ali Iddi katikati akiwa na wakuu wa Chuo cha ZCBE kisiwani Pemba, pamoja na
mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla mwenye mkoba,
wakiingia katika viwanja vya mahafali ya kwanza ya chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WANANCHI mbali mbali na viongozi wa serikali
wakiongozwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Pemba,Mhe:Ali
Nassor Mohamed wakimsikiliza kwa makini Balozi Sief Sharif Hamad wakati akitoa
hutuba yake, katika mahafali ya kwanza ya chuo cha ZCBE kisiwani Pemba. .(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiwemo maafisa
wadhamini kutoka ofisi mbali mbali, maafisa Tawala na wawakilishi wa kuteuliwa,
wakimsikiliza Balozi Seif Ali Iddi wakati alipokuwa akitoahutuba yake katika
mahafali ya kwanza ya chuo cha ZCBE kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWENYEKITI wa baraza la Chuo Cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E) kisiwani Pemba, Mhe:Hemed Suleiman Abdalla akitoa maelezo ya chuo kwa wageni mbali mbali waliohudhuria mahafali ya kwanza ya Chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid
Abdalla, akizungunza katika mahafali ya Kwanza ya chuo cha Zanzibar College Of
Business Education (Z.C.B.E) kisiwani Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAHITIMU wa fani ya Manunuzi
na Ugavi wa Chuo cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E) kisiwani
Pemba, wakivaa kofia zao baada ya kutunukiwa astashahada zao na Makamo wa Pili
wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi wakati wa mahafali ya kwanza ya
chuo hicho.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
WAHITIMU wa fani mbali mbali
katika chuo cha Zanzibar College Of Business Education (Z.C.B.E)Kisiwani Pemba,
wakiwa na huzuni baada ya kutunukiwa astashahada zao na Makamo wa Pili wa Rais
wa Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo
hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MAKAMO wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Mhe:Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi cheti na fedha shilingi laki
mbili, mwanafunzi Mohammed Suleiman Khalfan, baada ya kuibuka mwanafunzi bora
katika fani ya Uhasibu, wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Z.C.B.E
Kisiwani Pemb.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
No comments:
Post a Comment