Habari za Punde

NMB yamwaga misaada Hospitali ya Mnazimmoja na skuli ya Mwanakwerekwe


Afisa Mkuu Fedha NMB, Waziri Barnabas akikabidhi vitanda vya kujifungulia wakina mama wajawazito katibu mkuu wa wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ali Abdalla kwaajili ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Z’bar.
NMB imetoa msaada wa zaidi ya madawati 50 kwa ajili ya kusaidia shule ya msingi Mwanakwerekwe E na vitanda vya wagonjwa kwa ajili ya hospitali ya mnazi mmoja, misaada yote ikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 10.

Afisa Mkuu Fedha wa NMB, Waziri Barnabas alisema msaada huo ni mwitikio wa NMB kusaidiana na wananchi pamoja na serikali katika kutatua changamoto za elimu na afya nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Asha Ali Abdalla alipokea vifaa vya hospitali kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kuishukuru benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu na afya.
Waziri Barnabas akiwaelekeza jambo wanafunzi wa shule ya msingi Mwanakwerekwe E baada ya NMB kukabidhi msaada wa madawati 50.
Waziri Barnabas akikabidhi madawati kwa wanafunzi. 
Credit:MillardAyo.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.