Habari za Punde

Wavamizi na wamiliki wa ardhi kinyume cha Sheria Dar wakumbwa na bomoabomoa

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Alphayo Kidata (kulia) akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni  jana jijini la Dar es salaam.Kulia ni Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bw. Alphayo Kidata  (hayupo pichani) alipokuwa akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo yanayomilikiwa kisheria na watu wengine katika manispaa ya Kinondoni  jana jijini Dar es salaam
Moja ya ukuta uliojengwa kinyume cha sheria katika eneo lisiloruhusiwa eneo la Tegeta ukibomolewa jana

Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika maduka eneo la Tegeta Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam. 

Fundi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) akiendelea na zoezi la kukata umeme eneo la Mikocheni B kufuatia zoezi la bomoa bomoa lililokuwa likiendeshwa  na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Manispaa ya Kinondoni, jana jijini Dar es salaam.

Tingatinga likiendelea kubomoa maduka eneo la Tegeta Machakani kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.

Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wa zoezi la bomoa bomoa maeneo ya wazi na yale yaliyochukuliwa kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi wanaoyamiliki kihalali eneo la Mikocheni na Tegeta jijini Dar es salaam.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.