Waziri Mbarouk Afanya ziara Kituo cha Kurushia Matangazo ya Redio Bungi

Ni Mnara wa kurushia matangazo wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ulioko Bungi Wilaya ya Kati Unguja. 
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Said Mbarouk akimsikiliza Fundi Mkuu wa ZBC Redio Ali About Talib, akitowa maelezo ya ufanisi wa kituo cha kurushia matangazo ya Reduio Bungi Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea kituo hicho.  
Mkurenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Nd. Hassan Abdalla Mitawi akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Said Ali Mbarouk, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ZBC alipofika kituo cha kurushia matangazo cha ZBC Redio Bungu Zanzibar. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk akikagua Jenereta linalotarajiwa kutumika pindi umeme utakapokosekana kituoni hapo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kumaliza ziara yake kituoni hapo. (Picha na Miza Othman Maelezo-Zanzibar).

Post a Comment

Previous Post Next Post