Habari za Punde

Maadhimishi ya Wiki ya Maji Dar.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki  na Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika wakifungua maji ya bomba kwenye Zahanati ya Kijiji cha Mpiji Magohe mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji hicho manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua mradi wa maji uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 460 katika kijiji cha Mpiji Magohe, manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam leo wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayoendelea mkoani Dar es salaam.Kushoto kwake ni Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua Tenki la kuhifadhia maji  katika kijiji cha Mpiji Magohe, manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam leo wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayoendelea mkoani Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mpiji Magohe Kata ya Mbezi, manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji hicho leo.
 Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika akizungumza na wa kijiji cha Mpiji Magohe Kata ya Mbezi, manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji hicho leo.( Photo/Aron Msigwa -MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.