Habari za Punde

ZANTEL yawazawadia wateja wake kupitia promosheni ya “Kwangua Ushinde”

Bw. Ikirima Mattar Nassor (54) wa Kajificheni Ngome Kongwe (K), akipokea zawadi yake kutoka kwa Bw. Mohamed Mussa, Mratibu wa mahusiano ya serikali ZANTEL

ZANTEL ilizindua promosheni ya “Kwangua Ushinde” kwa lengo la kuwazawadia wateja wake na wateja wapya jijini Zanzibar. Zawadi zilizotolewa ni pamoja na Majokofu, simu aina ya Samsung na muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi elfu kumi (10000/=) kila wiki kwa wiki kumi na mbili mfululizo.

Kushiriki katika droo hiyo wateja wa ZANTEL walitakiwa kuongeza muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 1000/= au zaidi kwa kununua vocha  au kupitia huduma ya MIMINA itolewayo na ZANTEL, kwa kufanya hivyo mteja anaingia kwenye droo ya “Kwangua na Ushinde” moja kwa moja na kupata  nafasi ya kujishindia zawadi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa mahusiano ya serikali wa ZANTEL, Mr Mohamed Mussa alisema “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wateja wetu kwa kuchagua mtandao wa ZANTEL ambao unatoa huduma bora na nafuu zaidi nchini.

Washindi wetu wa promosheni hii wamefurahia zawadi zao walizopewa kwa wakati muafaka na kama tulivyowaahidi.

Mussa, amewapongeza washindi wote wa promosheni ya “Kwangua Ushinde” na kuongeza kuwa kampuni ya ZANTEL inaamini zawadi zilizotolewa zinalenga katika kuwakwamua wateja wake kimaisha na kuleta maendeleo kwa jamii nzima kwa ujumla.


Promosheni ya “Kwangua Ushinde” imeisha rasmi na tunatoa wito kwa wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu bora na nafuu zinazotolewa na kampuni ya simu ya ZANTEL,” aliongeza Mussa

Mshindi wa jokofu Ndugu Ikirima Mattar Nassor (54) wa Kajificheni, Ngome Kongwe alisema “Nilijua kuhusu promosheni hii lakini sikuitilia maanani na hivyo niliendelea kuweka vocha kama desturi yangu na kutumia. Bila kutegemea nimekuwa mmoja kati ya washindi wa jokofu. 

Naishukuru kampuni ya simu ya ZANTEL kwa kuendesha promosheni hii,” Nassor alipoulizwa anawaambia nini wateja wengine wa ZANTEL alisema, “Kwa kweli sasa naamini kuwa mteja yeyote wa ZANTEL anaweza kushinda kwenye promosheni zinazoendeshwa na kampuni ya ZANTEL. Hivyo nawashauri wateja wa ZANTEL kushiriki kikamilifu kwenye promosheni zijazo,” alimaza Nassor.


ZANTEL imekuwa mstari wa mbele katika kubadilisha mfumo wa mawasiliano Zanzibar kwa kubuni huduma ambazo zimekuwa zikiboresha maisha ya wananchi wa Zanzibar siku hadi siku. Huduma hizi ni pamoja na TUKUZA inayowawezesha wateja wa ZANTEL kununua umeme na huduma nyingine nafuu.

ZANTEL ni mdau mkubwa wa mradi wa “Afya ya Mama na Mtoto” (Wazazi Nipendeni), unaosimamiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na programu ya CDC.


ZANTEL imetunukiwa tuzo ya ushiriki katika muungano wa makampuni binafsi wenye lengo la kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ungonjwa hatari wa Malaria Tanzania. Programu hii inafanya kazi kwa karibu na wafanyakazi, familia na jamii kwa ujumla katika nguzo kuu nne: Kuzuia, Kuelimisha, Ushawishi na Uenezi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.