Habari za Punde

Dk Shein: Serikali itaendelea kushirikiana na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Maliasili cha Benki ya ADB  BibiSheila Khama  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Mwakilishi Mkaazi wa Benki hiyo nchini Tanzania Bi Tonia Kandiero,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Maliasili cha Benki ya ADB Bibi Sheila Khama (katikati) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Mwakilishi Mkaazi wa Benki hiyo nchini Tanzania Bi Tonia Kandiero(kushoto),[Picha na Ikulu.] 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Mkurugenzi wa Kituo cha Maliasili cha Benki ya ADB BibiSheila Khama baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Mwakilishi Mkaazi wa Benki hiyo nchini Tanzania Bi Tonia Kandiero,[Picha na Ikulu.]

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                       06 Mei, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameihakikishia Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Benki hiyo kwa kuwa mara zote imekuwa tayari kuunga mkono jitihada za Serikali za kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Maliasili cha Benki hiyo Bibi Sheila Khama Ikulu leo, Dk. Shein amesema amevutia sana na utayari wa benki hiyo wa kushirikiana na serikali katika jitihada zake za kuendeleza sekta mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Dk. Shein alimwambia Bibi Sheila kuwa matokeo ya ushirikiano kati ya benki hiyo na Zanzibar katika baadhi ya sekta yamezidi matarajio hivyo aliipongeza na kuishukuru kwa ushirikiano wake huo na mafanikio hayo.


Kwa hivyo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimueleza Mkurugenzi huyo wa Kituo cha Maliasili cha ADB kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Benki hiyo katika sekta nyingine kwa manufaa ya watu wa Zanzibar.

Benki ya Maendeleo ya Afrika imekuwa ikishirikiana na Serikli ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi mbalimbali kwenye sekta ya afya, maji, barabara, elimu na utawala bora.

Kwa upande wake Bibi Sheila Khama alimueleza Mheshimiwa Rais kuwa dhamira ya Benki yake ni kuona inaimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta zinazoshirikiana hivi sasa na kuanzisha ushirikiano katika sekta nyingine zaidi za uchumi na maendeleo ikiwemo sekta ya nishati.

Bibi Sheila Khama ambaye alikuwa amefuatana na Mwakilishi Mkaazi wa Benki hiyo nchini Tanzania Bi Tonia Kandiero amesifu ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Benki yake jambo ambalo limewezesha Benki hiyo kufanya shughuli zake kwa mafanikio humu nchini.


Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

                                               

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.