Habari za Punde

Wakulima wa viazi Makangale walia na wadudu waharibifu


Na Haji Nassor, Pemba                 
WAKULIMA wa zao la viazi shehia ya Makangaale wilaya ya Micheweni Pemba, wameitaka wizara ya kilimo kufanya utafiti wa haraka na wakina, ili kujua chanzo za viazi wanavyolima kuingia wadudu kwa kila msimu.
Walisema imekuwa ni jambo la kawaida katika miaka ya hivi karibuni, kushuhudia viazi kuwa na wadudu, jambo ambalo huwarejesha nyuma na hasa kwa vile walikuwa na utamaduni wa kuviweka vaizi kwa muda mrefu kwa ajili ya matumizi baada ya mavuno.
Kwa sasa wakulima hao hukosa kujiwekea akiba ya viazi hivyo kutokana na kutawaliwa na wadudu, na ndio maana wakaishauri wizara husika kuangalia uwezo wa kufanya utafti wa kina, ili wawe na njia mahasusi ya kilimo hicho na kuondokana na wadudu hao.
Wakizungumza na mwandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wakulima hao walisema wakati umefika kwa Idara inayoshughulikia mazo ya chakula na biashara, kukaa na wakulima hao, ili kuibua changamoto ya kitaalamu inayosababisha hali hiyo.
Mkulima Hamad Kombo, alisema kwmauda mrefu yeye anajishughulisha na kilimo hicho, ingawa ni miaka mitano ya hivi karibuni ndio kumijitokeza wa dudu hao.

“Hawa wadudu wamezuka hivi karubuni na sisi tulidhani ni kutokana na upepo mkali, ambao husambaaza mauwa ya miti mingi na yanapoanguka kwenye shamba la viazi huzaa wadudu’’,alifafanua.
Nae mkulima Aisha Hassan Ali, alisema wadudu hao aina ya funza waupe na kijani wamekuwa wakijitokeza kwenye viazi hasa wakati wa kukaribia kuvuna, ingawa sio wengi sana kwenye shamba lake.
Kwa upande wake Mathias Charles alisema, ni vyema wataalamu wa idara ya kilimo wakajikita kwenye kuwapatia dawa au kufanya utafiti ili wagundue tatizo linalosababisha hali hiyo.
Akizungumzia hilo, Afisa mkuu wa taasisi ya utafiti na kilimo Pemba Idrissa Haasan Abdalla, alisema tayari wameshapokea malalamiko hayo na mengine na watayafanyia kazi.
Alisema ukosefu wa vifaa vya uhakika kwenye maabara ya kilimo, likiambatabana na kokosa fungu maalumu la fedha la kuendeshea tatfiti, ndio changamoto kubwa inayorejesha nyuma kazi zao.
“Unajua huwezi kufanya utafiti kwa kutegemea fedha za matumizi ya ofisi, lazima tuwe na fungu maalumu, huwezi kufanya utafiti kwa shilingi laki 7, lazima kuwe na fedha itatua kila kitu’’,alisema.
Hata hivyo alisema wamekuwa na utaratibu baadhi ya tafiti zao kuzihamishia Unguja kwenye maabara ya kilimo ambayo inavifaa kamili, na hawasiti kufanya kazi zao licha ya changamaoto hizo.
Katika hatua nyengine alisema huwezi kukurupuka kutoa majibu ya kitaalamu panapojitokeza jambo linalohitajika kufanyia utafiti, ingawa alisema wadudu wa aina hiyo hujitokeza wakati wa jua kali.

Eneo la Makangale wilaya ya Micheweni ni maarufu kutokana na ukulima wa zao la  viazi na ndio ambalo linawaletea maendeleo endelevu kwenye chakula na biashaara na wakaazi wengine wakielekeza nguvu kwenye uvuvi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.