6/recent/ticker-posts

Harakati za Maandalizi ya Kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Hajj Zenj.

 Msongomano wa magari katika eneo la marikiti kuu Darajani wakati wa kipindi hichi cha sikukuu kama inavyoonekana katika Taswira yake hiyo.

                             Taswira ya Dada Njoo Jua Kali Darajani ikionekana
 Taswira ya darajani Jua Kali au Dada Njoo wananchi walivyojitokeza kufuata mahitaji ya Watoto wao maeneo hayo maarufu Zenj kwa bidhaa za vitambaa na nguo za watoto.

 Hivi ndivyo ilivyokuwa katika maeneo ya jua kali Darajani wananchi wa Zanzibar wakikamilisha mahitaji ya Watoto wao ili kuweza kushiriki vizuri kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj Zanzibar kuungana na Waislam wengine Duniani 
 Wananchi Zanzibar wakifanya maandalizi ya maakuli ili kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakinunua mbatata kati soko kuu Darajani juzi. Mbatata kilo moja iliuzwa shilingi 1000/= kwa kilo na kitunguu maji kilo moja iliuzwa shilingi 1500/=
Wananchi kisiwani Zanzibar wakiwa katika harakati za kujipatia mahitaji yao kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj ilioadhimishwa duniani kote baada ya Ibada ya Hijja inayofanyika Nchini Saudi Arabia. 

Post a Comment

0 Comments