Habari za Punde

Zoezi la Kutangaza Matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar likiendelea katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Bwawani Zanzibar.

Wananchi na Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wakiwa katika Ukumbi wa Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika Ukumbi wa Salama wakisubiri kutangazwa kwa Matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe.Jaji Abdulhakim Ameir Issa akitangaza Matokeo ya Wagombea Urais wa Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar mchana huu. akitakaza Matokeo ya Kura za Majimbo 18 ya Uchaguzi Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jaji Abdulhakim Ameir Issa akitangaza matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar mchana huu.
 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe. Jecha Salum Jecha akiwa na Makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC katika ukumbi wa Salama Bwawani wakati wa kutangazwa kwa Matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar yakitangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jaji Abdulhakim Ameir Issa. 
Mawakala wa Wagombea Urais wa Zanzibar wakifuatilia matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar yakitangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jaji Abdulhakim Ameir Issa, katika Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar. 
Waangalizi wa Kimataifa wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2015, wakati ya utoaji wa matokeo hayo yanayotolewa katika ukumbi wa Salama Bwani Zanzibar na Tume ya Uchaguzi Zanzibar. 
Mawakala wa Vyama vya Siasa wakifuatilia Matokea ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar katika Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar mchana huu.
Mawakala wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani wakifuatilia matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar  wakati yakitangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jaji Abdulhakim Ameir Issa.
Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wakiwa katika Ukumbi wa Afisi za Tume Bwawani wakati wa kutolewa kwa Matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar.
Mtaalamu wa alama za lugha za Watu Wenye Ulemavu wa Kutokusikia (VIZIWI) akitowa ishara za lugha kwa ishara wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya Kura katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika Ukumbi wa Salama wakifuatilia Matokeo ya Kura za Wagombea Urais wa Zanzibar yakitangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar katika Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.