Habari za Punde

Mhe. Luhaga Mpina Atembelea Kituo cha Afya Fuoni Kibondeni na Skuli ya Msingi Kitongani Fuoni Kuangalia Ahadi ya Ujenzi wa Madarasa ya Skuli hiyo Yaliotolewa Ahani na Rais Mstaaf Jakaya Kikwete.

Kituo cha Afya kilioko Fuoni Kibondeni ambacho kilitembelewa na Mhe Luhaga Mpina katika Jimbo la Dimani kikiwa ni moja ya kero kwa Wananchi wa kituo hicho kwa kudai kiko mbali na njia yake kuwa mbaya na shinda kufika Wananchi kupata huduma za afya kituoni hapo na kumuomba Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mizingira kuwafanyia utaratibu wa kuwatengenezea barabara hiyi kuwa rahisi kufika Wananchu kupata huduma za Afya na kupatiwa vifaa kwa ajili ya kituo hicho, Kikiwa na Hudumna zote za Uzazi kulaza waginjwa na jengo la kuhifadhia maiti.Kituo hicho kilizinduliwa na Aliyekuwa Waziri Kiongozi Mstaaf Mhe Shamsi Vuai Nahodha mwaka 2004.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina akitembelea kituo hicho na kupata maelezo kutoka kwa Daktari Dhamani Ndg Said Amour wakati alipofika kituoni hapo akiwa katika ziara yake.

Afisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira. Mhe Luhaga Mpina wakiwa katika chumba cha kuzalia Wakinamama katika Kituo hicho lakini hakifanyi kazi kwa kukosa Vifaa.
Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shughuli za Uratibu Muungano Ndg Issa Ibrahim, akipata maelezo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Mhe.Hafidh Ali Tahir wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Muungano Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara zake Kisiwani Zanzibar kutembelea miradi mbalimbali ilioko chini ya Muungano. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akitembelea jengo la Kituo cha Afya Fuoni Kibondeni Zanzibar.
 Naibu Waziri akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed, alipofika kukitembelea kituo hicho cha Afya na Mbunge wa Jimbo hilo la Dimani Mhe Hafidh Ali Tahir.

Mhe Luhaga Mpina akipata maelezo alipotembelea jengo la kuhifadhia maiti la kituo hicho cha Afya Fuani Kibondeni.

  Jengo la kuhifadhia maiti la kituo hicho cha Fuoni Kibondeni.
Mbunge wa Jimbo la Dimani Mhe Hafidh Ali Tahir akizungumza wakati wa ziara ya Mhe. Lihuga Mpina katika Jimbo lake.

Maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakiwa katika msafara wa Mhe Naibu Waziri 
Ofisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed akitowa maelezo ya Kituo hicho cha Afya Fuoni Kibondeni Zanzibar Jimbo la Dimani. 
Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Ndg Bakari Rajab akijitambulisha kwa Wananchi wa Jimbo la Dimani wakati wa ziara ya Naibu Waziri katika Jimbo hilo.
Mkurugenzi Uratibu Muungano Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg Issa Ibrahim akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Dimani. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Dimani alipofika kuwatembelea na kuagalia Kituo chao cha Afya kuona namna ya kukisaidia Kituo hicho kwa ajili ya kuimarisha utowaji wake wa huduza za Afya kwa Wananchi wa Jimbo hilo na jirani na kuahidi kukiimarisha  kwa kukipatia baadhi ya vifaa kuweza kutowa huduma.kwa ufanisi zaidi. 
Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Dimani wakimsikiliza Naibu Waziri alipofika kuwatembelea wakati wa ziara yake Zanzibar.
Afisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed, akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina wakati alipofika katika Skuli ya Msingi ya Fuoni Kitogani ikiwa ni moja ya Ahadi za Rais Mstaaf wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete alipofika katika Skuli hiyo na kutowa ahadi ya kumalizia Ujenzi wa Madarasa ya Skuli hiyo. 
Mbunge wa Jimbo la Dimani Mhe Hafidh Ali akitowa maelezo ya Jimbo hilo akiwa na ramani ya Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA ya uchimbaji wa Visima viwili ambavyo tayari vimeshachimbwa na kutoa huduma kwa Wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akitowa maelezo kwa Wananchi wa Jimbo la Dimani wa Kamati ya Skuli ya Kitongani Fuoni baada ya kupokea maelezo yao ya Ahadi ya Rais Mstaaf  wa Tanzania Dk JK alipofika katika Skuli hiyo, wakati wa ziara yake Zanzibar. Naibu Waziri amesema atazishughulikia kero zao hizo, baada ya kusema kero zao ni barabara kisima kwa ajili ya skuli hiyo na kituo cha afya. 
Mbunge wa Jimbo la Dimani Mhe. Hafidh Ali Tahir,akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Luhaga Mpina alipofika katika skuli hiyo wakati wa ziara yake Zanzibar. 


Afisa wa Mamlaka ya Maji Zanzibar akimuonesha sehemu ya eneo hilo lililochimbwa visima viwili kwa kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Jimbo hilo 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.