Habari za Punde

Michuano ya Bingwa Mafunzo na AS Vita Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan. Timu ya AS Vita Imeshinda 3--0

Wapenzi wa Mchezo wa Soka Zanzibar wakishangilia Timu yao ya Mafunzo Inayoshiriki Michuano ya CAF mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar katika mchezo huo Timu ya AS Vita Club imeshinda mchezo huo bao 3--0.
Katika Mchezo huo timu ya AS Vita imepata mabao yao katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo yaliofungwa na Wachezaji katika dakika ya tano ya mchezo huo Mshambuliaji Ikanga Manymona ameipatia bao timu yake kwa shuti la mbali nje boksi , mshambuliaji huo kwa mara ya pili ameiandikia balo la pili katika dakika ya 29 ya mchezo huo kwa kuunganisha mpira wa krosi na bao la kufunga ushindi wa Timu ya AS Vita limefungwa na mshambuliaji Ngonda Mazinga katika dakika ya 44 ya mchezo huo na kufunga karamu ya magoli katika mchezo huo, uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Nae Kocha Mkuu wa timu ya Mafunzo Hemed Moroco amesema timu yake imecheza vizuri mchezo huo tatizo kwa wachezaji wake ilikuwa wamecheza na timu yalikuwa hawakuijua mchezo wao na kuweza kufungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo Baada ya kuutambua mchezo wao wameweza kuzuiya na kushambulia lakini bahati haikuwa yao katika mchezo huo timu yake imeonesha mchezo mzuri.  

Viongozi wa Serikali na Vyama vya michezo wakifuatilia mchezo huo wa Kombe la Mapingwa kati ya Mafunzo na Timu ya AS Vita Club ya DRC mchezo umefanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Wachezaji wa Timu ya Mafunzo na AS Vita wakiwa katika mchezo huo wa Kombe la Mapingwa uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mshambuliaji wa Timu ya AS Vita akimuliki mpira wakati wa mchezo waho huo. 
Beki wa timu ya AS Vita Landu Pauat akiokoa mpira huku mshambuliaji wa timu ya Mafunzo Jaku Juma akiwa tayari kuleta madhara katika, uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya AS Vita imeshinda bao 3--0 
Mshambuliaji wa Timu ya AS Vita Ikanga Manymona akiipatia bao la kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo huo kwa shuti la mbali nje na kumshinda mlinda mlango wa timu ya mafunzo na kuandia bap la kwanza kwa timu yake.
Beki wa Timu ya AS Vita akimiliki mpira wakati wa mchezo huyo.

Mashabiki wa Mchezio wa Soka Zanzibar wakishangilia Timu yao ya Mafunzo inayoshiriki Kombe la Mabingwa la CAF mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.