KUKANUSHA UPOTOSHAJI DHIDI YANGU
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Kumekuwa na upotoshwaji wa taarifa zinazosambaa juu ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, na Mkuuwa Wilaya ya Wanging'ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela, ambapo baadhi ya vyombo vya habari kama Magazeti na mitandao ya kijamii vimekuwa viripoti tofauti.
Akizungumza na mtandao huu, wa Sufianimafoto.com kwa njia ya simu, Mwakalebela alisema kuwa zimekuwepo taarifa za upotoshwaji dhidi yake baada ya kuibuka kesi ya mtuhumiwa aliyepandishwa Kizimbani mwenye jina linalofanana na lake mwenye jina la David John Mwakalebela (56).
Aidha Mwakalebela alisema kuwa Mtuhumiwa huyo, aliyewahi kuichezea timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, na timu ya Taifa, wakati yeye akiwa ni Katibu Mkuu wa TFF, alipandishwa kizimbani yeye na aliyewahi kuwa Mr. Tanzania 2015, Muhammad Khalil (32) wakikabiliwa na mashitaka saba likiwemo la kuishi nchini bila kibali na kumsaidia Mshitakiwa kutoa taarifa za uongo.
Kutokana na kufanana kwa majina hayo,kumekuwepo na sintofahamu na usumbufu mkubwa kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya huyo ya Wanging'ombe huku ndugu, jamaa na marafiki wakihaha huku na huko na wengine wakimpigia simu kwa mshituko, jambo ambalo si la kweli.
''Zimeene taarifa potofu juu yangu zikielekeza tuhuma hizo dhidi yangu kwa makusudi au kwa kutofahamu jambo ambalo ni Hatari kwa Mimi binafsi, familia na marafiki kwa ujumla, nawaomba wahusika wawe wakifuatilia undani wa stori yenyewe ili kupata uhakika kabla ya kuanza kueneza uzushi na kuzua taflani,
Aidha napenda kuwapa pole wanafamilia yangu, ndugu, jamaa na marafiki kwa usumbufu wote uliojitokeza kwao kutokana na sintofahamu hii na kusababisha kadhia dhidi yako". alisema Mwakalebela
Mtuhumiwa David Mwakalebela, akiwasili Mahakamani,ambaye amefananishwa na Fredrick Mwakalebela.
No comments:
Post a Comment