Na: Abubakar Kisandu,
Raisi wa heshima wa mchezo wa Judo
Zanzibar mwenye asili ya Japan Abdul
Maalim Shimaoka alitoa ahadi kwa Wazanzibar ya kufanya
vizuri katika mashindano ya kumi ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika tarehe 26-27 ya mwezi huu mjini Bunjubura nchini Burundi.
Alisema wamejiandaa vizuri licha ya vikwazo mbali mbali walivyokumbana navyo ikiwemo mambo ya siasa na anaamini vijana wake watarudi na ubingwa.
“Tulifanya maandalizi ya mwezi mzima kwa kujiandaa na mashindano haya, vijana wangu wana ari sana na malengo yao ni kufanikiwa kufika mbali katika mchezo huu wa Judo”.
Mbali na hayo Shimaoka alisema kitu chengine anachojivunia ni wachezaji wake watatu waliopata Mafunzo ya Judo nchini Japan kuanzia mwezi Septemba hadi Disemba mwaka jana 2015, hivyo anaamini watarudi na kombe Zanzibar kutoka huko Burundi.
“ Najivunia wachezaji wangu watatu waliopata mafunzo kule Ali Juma, Hafidh Makame na Mbarouk Suleiman”.
Miongoni mwa wachezaji hao yupo pia Salma Omar
ambaye anacheza uzito wa kilo 52 mwanamke pekee
kwa mwaka huu kutoka Zanzibar kwenda katika Mashindano hayo huko Burundi.
“Nina imani kwa jinsi nilivyo fanya mazoezi nitashinda tu, kimazoezi nipo sawa, nidhamu ninayo ya hali ya juu, walimu wananiamini pia nimejifunza kutokana na makosa ya miaka ya nyuma, hivyo hakuna sababu ya kuwa nisifanye vizuri”.
Katika mashindano hayo Zanzibar imepeleka wawakilishi watakao shindana wakiwa na uzito tofauti wakiwemo Azan Hussein na Ali Juma ambao watashiriki kwa uzito wa kilo 60.
Abdul rabi Alawi na Mansabu Alawi ni ndugu watacheza kwa uzito wa kilo 66. Na kwa upande wa uzito wa kilo 73 yupo Hafidh Makame pekee ambapo kwa uzito wa kilo 81 atawakilisha Mbarouk Suleiman, wakati huo huo Rajab Kassim atashiriki kwa wenye uzito wa kilo 90 na Masoud Amour yeye atashiriki uzito wa kilo 100.
Mohd Abdul rahman na Iddi Othman watashindanauzito wa zaidi ya kilo 100.
No comments:
Post a Comment