Habari za Punde

Balozi Seif Aweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Kwarara na Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Tumaini

Mandhari ya eneo linalojengwa Skuli ya Ghorofa  kwarara pamoja na Kituo cha Habari na Mawasliniano cha Tumaini Wilaya ya Magharibi “B” unaofadhiliwa kwa pamoja kati ya mashirikia matatu ya Good Neighbors,  Shirika la Habari la Korea Kusini {SBS } pamoja na Shirika la Maendeleo ya Korea Kusini KOICA.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Skuli ya Ghorofa  na Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Tumaini hapo Kwarara Wilaya ya Magharibi.
Msimamizi wa Ujenzi wa Skuli mpya ya Ghorofa ya Kwarara Mhandisi Ali Mrabouk akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ramani ya ujenzi wa  majengo ya Skuli ya Ghorofa ya Kwarara pamoja na Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Tumaini.
Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Bwana Songo akitoa salamu kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Skuli ya Ghorofa pamoja na Kituo cha Habari na Mawasiliano zinazojengwa kwa msaada wa mashirika ya Nchi hiyo.
Wanafunzi wa skuli za msingi wanaosoma kwenye shehia ya Kwarara wakishangiria matukio mbali mbali kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya ghorofa ya eneo hilo.(Picha na – OMPR – ZNZ.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.