JENGO ambalo lilikuwa kituo cha Afya cha Kiuyu
Minunwini, ambalo kwa sasa lilikuwa limehifadhiwa dawa zilizokuwa zimepitwa na
muda, vitabu vya skuli ya Minungwini, limeteketea lote kwa moto, usiku wa
kuamkia Machi 12 mwaka huu, moto uliosadikiwa kutiwa majira ya saa 10: 00
alfajiri, na kufanya idadi ya matukio hayo kufikia nane Kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
TAWI la Chama Cha Mapinduzi CCM Tibirinzi
wilaya ya Chake chake, likiwa limekumbwa na zahma ya kuungua moto, ambapo moto
huo umejumuisha matukio nane kisiwani Pemba yalioripotiwa kutokezea usiku wa
kuamkia Machi 12 kisiwani humo, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment