Habari za Punde

Mchezo wa Timu ya JKU na Villa Kuchezeshwa na Waamuzi kutoka Djibouti.

Kikosi cha Timu ya JKU Kinachojiandaa katika mchezo wake wa raundi ya Pili ya Michuano ya CAF na Timu ya SA Vila ya Uganda.

Na Mwandishi Wetu.
Shirikisho la kabumbu barani Afrika(CAF) limewateuwa waamuzi wenye beji za FIFA kutoka nchini Djibouti kuchezesha pambano la awali kati ya Sports Club Villa Jogoo ya Uganda dhidi JKU ya Zanzibar.

Kupitia Shirikisho lao la mpira nchini Uganda (FUFA) Sports Club Villa tayari wamethibitisha kuwa pambano hilo litachezwa kwenye dimba la kimataifa la Mandela Jumamosi ya March 12 saa kumi alasiri.

Waamuzi hao ni Souleiman Ahmed Djamal, Abdillahi Mahamoud Iltireh, Hamze Abdi Salime, Djamal Aden Abdi na Kamisaa wa mchezo huo atakua Aweis Ahmed Jumal kutoka nchini Somalia.

Sports Club Villa imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa Al Khartoum ya Sudan kwa ushindi wa jumla ya 2-0 kufuatia michezo miwili waliocheza.

Kwa upande wao JKU walifanikiwa kuingia nafasi hiyo bilaya jasho kutokana na wapinzani wao Gaborone United
kutoka Botswana kujiengua kwenye kombe hilo la Shirikisho barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.