Habari za Punde

Shamra shamra za kusherehekea ushindi mkubwa wa CCM zimeanza

 Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akikabidhiwa Hati ya kumthibitisha kwamba ameshinda uchaguzi  Jimbo hilo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu Khamis aliyepo kati kati.

Wa kwanza kutoka kulia ni Msaidizi  Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya Kaskazini “B” Nd. Abdulla Bakar Khamis na kulia ya Nd. Pandu ni msaidizi  Msimamizi wa Pili wa Uchaguzi wa Wilaya hiyo Bibi Maryam Majid Suleiman.
 Balozi Seif akionyesha hati yake aliyokabidhiwa mara baada ya kushinda uchaguzi Jimbo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu Khamis  akimkabidhi hati ya Ushindi Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Kiwengwa Bibi Asha Abdulla Mussa  hapo Skuli ya Sekondari ya Mahonda.

 Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Bumbwini Bibi Mtumwa Pea Yussuf akionyesha kwa furaha Hati yake iliyomthibitisha kuwa ameshinda Uchaguzi katika Jimbo hilo kupitia chama cha Mapinduzi.

Picha na –OMPR – ZNZ.

Shamra shamra za kusherehekea ushindi kufuatia kukamilika kwa Uchaguzi wa Marejeo uliokipa nafasi chama cha Mapinduzi kuendelea kuongoza Dola zimeanza katika maeneo mbali mbali Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.

Furaha hizo zilianza mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Jecha Salum Jecha kutangaza washindi kwenye kinyang’anyiro hicho hapo katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.

Sherehe hizo zilikwenda sambamba na wawakilishi pamoja na madiwani wateule kwenye majimbo na wadi kukabidhiwa vyeti vyao vya ushindi na maafisa wa Tume ya Uchaguzi wa Wilaya.

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu Khamis alikabidhi vyeti kwa washindi  wateule wa Majimbo na Wadi zilizomo  ndani ya Wilaya ya hiyo hafla hiliyofanyika katika uwanja wa Skuli ya Sekondari ya Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unaguja.

Waliokabidhiwa vyeti hivyo ni Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Mahonda ambae pia ni makamu wa Pili wa Raisw wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Bibi Asha Abdulla Muusa Mwakilishi mteule wa Jimbo la Kiwengwa pamoja na Mwakilishi mteule wa Jimbo la Bumbwini Bibi Mtumwa Pea Yussuf.


Dr. Khalid Salum Mohammed  ni Mwakilishi Mteule wa wa Jimbo la Donge ambae alidharurika katika hafla hiyo fupi.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wawakilishi na Madiwani wateule wa Majimbo na Wadi zilizomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” wakati wa kusherehekea ushindi huo hapo Ofisi ya CCM Wilaya  iliyopo Mahonda  Mwakilishi Mteule wa  Jimbo la Mahonda  

Balozi Seif Ali Iddi aliwashukuru Wanachama na Wananchi wa Majimbo ya Wilaya hiyo kwa umakini wao wa kuirejesha tena madarakani CCM .

Balozi Seif  pia aliwashukuru wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi 
pamoja na Mawakala wa vyama vya Siasa kwa kazi kubwa waliyoifanya iliyosaidia kuendeshwa kwa uchaguzi huo wa marejeo kwa amani na usalama.

Balozi Seif alisema jukumu walilobeba wasimamizi na mawakala hao limewawezesha wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi kupata haki zao katika uchaguzi huo kwa mujibu wa jinsi walivyonadi sera zao.

Wawakilishi na Madiwani hao wateule wa majimbo ya Wilaya ya Kaskazini “B” wameahidi kuwatumikia vyema wananchi wao katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

BaloziSeif aliwahakikishia wananchi wa Majimbo hayo kwamba kazi rasmi ya kuwatumikia inatarajiwa kuanza rasmi muda mfupi ujao mara baada ya kukamilika kwa taratibu wa kisheria.

Mwakilshi mteule huyo wa Jimbo la Mahonda waliwataka wanachama wa chama cha Mapinduzi kuwa waangalifu na kuchukuwa tahadhari wakati wote wa kusherehekea ushindi wao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.