Habari za Punde

Taarifa Kwa Wateja Wa ZECO Kwa Kukatika Kwa Umeme leo.

SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR ZECO LIMESEMA KUKATIKA KWA UMEME LEO KUMESABABISHWA NA HITILAFU ZA UMEME ZILIZOTOKEA KATIKA GRIDI YA TAIFA HUKO TANZANIA BARA.

MSAIDIZI AFISA UHUSIANO WA ZECO HAJI JUMA CHAPA AMESEMA KUWA  WAKATI WOTE AMBAO LIMETOKEA TATIZO HILO KUMESABABISHA KISIWA CHOTE CHA UNGUJA KUKOSA UMEME.

AMEFAHAMISHA KUWA UKOSEFU HUO ULIANZIA KUANZIA SAA TANO ZA ASUBUHI NA KURUDI SAA NANE MCHANA KUMESABABISHWA NA UPATIKANAJI MDOGO WA UMEME NA HATIMAE HUDUMA HIYO KUWEZA KUKOSEKANA KABISA.

HATA HIVYO AFISA HUYU AMEWAOMBA RADHI WANANCHI KWANI TATIZO HILO LILIKUWA LIKO NJE YA UWEZO WA ZECO.

WAKATI HUOHUO NDUGU CHAPA AMEWATOA HOFU WANANCHI WA ZANZIBAR KUTOKANA NA UVUMI WA SHIRIKA HILO KUTOKUUZA UMEME KATIKA KIPINDI CHA MARUDIO YA UCHAGUZI MKUU.

AMEFAFANUA KUWA HUDUMA YA KUUZA UMEME ITAENDELEA KUTOLEWA KAMA KAWAIDA ISIPOKUWA KWA SIKU ZA JUMAPILI NA JUMATATU VITUO VITAFUNGWA SAA 12 JIONI.

AMEWAOMBA WANANCHI KUPUUZIA TAARIFA ZOZOTE ZILE AMBAZO HAZITOKI KATIKA VYANZO HUSIKA NA KUENDELEA KUSIKILIZA VYOMBO VYA HABARI KWA TAARIFA ZENYE UHAKIKA.
  

Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano ZECO      18/03/2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.