Tarehe 8 March tunasherekea siku ya wanawake sasa tutakuwa na kampeni ya uwiano sawa wa kijinsia kuonyesha kuungana na Taasisi ya wanawake (TWA) ambao ndio waandaji rasmi wa kampeni hii ambayo itaambatana na matembezi tarehe 5 mgeni rasmi akiwa ni Mh Ummy Mwalimu ( Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,)
Na tarehe 6 tutakuwa na kongamano kujadili usawa wa kijinsia litakalofanyika Hyatt Regency Hotel Mgeni Rasmi akiwa ni Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu
link hii http://twa.or.tz/pledge/
Jumuika ńa #HatujafikaBado ńa utume ujumbe kuhamasisha upatikanaji wa #UwianoSawaKijinsia @TWAorg #PledgeForParity
No comments:
Post a Comment