Habari za Punde

Wananchi Zanzibar Wajitokeza Katika Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Uliofanyika 20,March 2016

 
 Mgombea Uwakilishi Jimbo la Tunguu Zanzibar Simai Mohammed Said akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo cha wapiga Kura Skuli ya Kibele Bungi Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja 
 Mawakala wa Vyama vya Siasa wakifuatilia majina ya Wapiga Kura katika Kituo cha Wapiga Kura cha Skuli ya Kibele Bungi Zanzibar wakati wa zoezi hilo la Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar. 
 Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakiagalia majina yao katika ubao maalum uliobandikwa picha za Wapiga Kura katika Kituo hicho Skuli ya Kitope Zanzibar.

 Mawakala wa Vyama vya Siasa Zanzibar wakifuatilia Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar katika Kituo cha Wapiga Kura Skuli ya Maandalizi Jangombe.
 Mwananchi wa Jimbo la Mpendae Zanzibar akitoka katika Kituo cha WEapiga Kura katika Skuli ya Maandalizi Jangombe Zanzibar.
 Mwananchi wa Jimbo la Mto Pope akipiga kura yake katika Kituo hicho. 
 Wananchi wa Jimbo la MtoPepo Zanzibar wakiagalia majina yao katika Kituo cha Kupigia Kura katika Skuli ya Mtopepo Zanzibar katika ubao maalum uliobandikwa picha za Wapiga Kura wa Jimbo hilo.
Mwananchi wa Jimbo la Mto Pepo Zanzibar akipata Karatasi ya Kupiga Kura katika Kituo cha Skuli ya MtoPepo Zanzibar kutoka kwa Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.