Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru Waanza Mbio Zake Wilaya ya Mjini Jimbo la Chumbuni Zanzibar.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake katika Jimbo la Chumbuni Zanzibar kwa kutembelea Miradi ya Wajasiriamali Wanawake wa Jimbo hilo na kukabidhi Fedha kwa Kikundi hicho cha Wajasiriamali.

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akizungumza wakati wa mbio hizo za Mwenge katika jimbo hilo na kuwahamasisha Wananchi katika miradi ya Maendeleo kwa Wananchi wa Jimbo hilo na kutowa mchango wao Mbunge na Mwakilishi kwa ajili ya Kikundi cha Wajasiriamali cha Mambo na Watu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg George Jaskson katikati akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chumbuni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya mbio za mwenge katika viwanja vya masumbani muembe makumbi. akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini.
 Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Miraj Khamis Mussa akimkabidhi Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg Goerge Jackson fedha kwa ajili ya Wajasiriamali wa Kikundi cha Mambo na Watu, zilizotolewa na Mwakilishi na Mbunge mchango wao kwa Kikundi hicho.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg Goerge Jackson akimpongeza Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Miraj Khamis Mussa kwa mchango wao kuwasaidia Wajasiriamali wa Kikundi cha Wanawake.
 
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg Goerge Jackson akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD)kwa mchango wao kuwasaidia Wajasiriamali wa Kikundi cha Wanawake.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg Goerge Jackson akimkabidhi fedha zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Muwezeshaji wa Wajasiriamali wa Jimbo la Chumbuni Mwanajuma Khatib Omar. wakati wa hafla hiyo ya mbio za mwenge katika Jimbo la Chumbuni katika viwanja vya masumbani.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakati wa mbio za Mwenge katika Jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.