Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Watembelea Shehia ya Shangani na Kuzungumza na Viongozi wa CCM wa Shehia Hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Tawi la Shangani Ndg Abdul Abeid akizungumza wakati wa Mkutano na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni walipofika katika Shehia hiyo kuzungumza na Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Kikwajuni, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Shangani Unguja.kulia Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Nassor Salim Jazira na kushoto Mbunge Mhe Hamaad Masauni.    
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe.Nassor Salum Jazira akizungumza na Viongozi wa Shehia ya Shangani Zanzibar wakati wa ziara yao kutembelea Wananchi wa Jimbo lao kujuwa kero zinazowakabili na kutimiza ahadi walizotowa.  
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Masauni akizungumza na Viongozi wa CCM wa Shehia ya Shangani wakati wa ziara yao kutembelea shehia hiyo na kuzungumza na Vjiongozi wa CCM katika ukumbi wa Tawi la CCM Shangani Zanzibar.   
Viongozi wa CCM Shehia ya Shangani Zanzibar wakimsikiliza Mbunge wakati wa mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Shangani Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.