Habari za Punde

Uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri na mabaraza ya miji kisiwani Pemba

 WAKURUGENZI wa Mabaraza ya Miji, Halmashauri na madiwani wa mikoa miwili ya Pemba, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akifanya uteuzi wa kuteuwa Wakurugenzi wapya wa mabaraza ya miji na Halmashauri pamoja na kuzindua madaraza ya madiwani Kisiwani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MKURUGENZI wa Baraza la Mji Wete Philipo Joseph akisoma ratiba za mkutano wa Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, Philipo kabla ya uteuzi huo alikuwa akifanya kazi ofisi kuu Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 AFISA Mdhamini ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Juma Nyasa Juma akitoa maelezo mafupi juu ya uzinduzi wa mabaraza ya madiwani Kisiwani Pemba,huko katika ukumbi wa kiwanja wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
 KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Radhia Rashid Haroub, akizungumza na madiwani, Wakurugenzi wa mabaraza ya Miji na Halmashauri kisiwani Pemba, kabla ya kufanya uteuzi wa wakurugenzi wapya na kuzindua baraza la madiwani Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MWENYEKITI wa Madiwani Wilaya ya Mkoani, Mwadini Ali Mwadini akitoa nasaha zake mara baada ya kuzinduliwa kwa mabaraza ya madiwani Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na madiwani, Wakurugenzi wa mabaraza ya Maji na Halmashauri Kisiwani Pemba, kabla ya waziri Haji Omar Kheri kuteuwa wakurugenzi wapya na kuzindua mabaraza ya madiwani Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akizungumza na madiwani, wakurugenzi wa mabaraza ya miji na Halmashauri Kisiwani Pemba, kabla ya kufanya uteuzi wa wakurugenzi wapya wa mabaraza ya miji na halmashauri na kuzindua baraza la madiwani Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akiwaonyesha madiwani sheria ambayo inayowaongoza uwepo wao, utendaji wao wa kazi za kila siku kabla ya kuzundua mabaraza ya madiwani Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Sueliman, PEMBA.)
 WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akitoa taarifa ya kuwateuwa wakurugenzi wa halmashauri na mabaraza ya miji kisiwani Pemba, kabla ya kuyazindua mabaraza ya madiwani kisiwani hapa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKURUGENZI wa Baraza la Mji Wete Philipo Joseph, akichukuwa dondoo za kikao kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la mji Wete.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.