Serikali ya Wilaya Chakechake Pemba kupiga marufuku uingaji wa gari za wanyama wakiwemo Ng'ombe eneo la mji, bado baadhi ya wamiliki wa gari hizo, wamekuwa wakipuuzia amri hiyo, ambapo camera ya Chombo hichi, imeinasa gari hiyo eneo la Tibiribnzi mkabala na Ikulu ya Chakechake, ikitokea mjini kuchukua bidhaa.
Jengo la Tawi la CCM Kisiwani Pemba eneo la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Pemba ambalo lilichomwa moto na Watu wasiojulikana hivi karibuni likiwa limekamilika ujenzi wake kama linavyoonekana picha, baada ya ujenzi huo kukamilika na kuaza kutumika kwa shughuli za Chama katika eneo hilo kwa Wanachama wake.(Picha na Haji Nassor, Pemba)
No comments:
Post a Comment