Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wafanya Ziara kutembelea Vyanzo vya Maji Jimbo Kuangalia Kero hiyo kwa Wananchi Wao.


Diwani wa Wadi ya Dunga Ussi akitowa maelezo ya moja ya chanzo cha Maji katika kisiwa cha Dungu kinachotowa huduma ya maji kwa Wananchi wa Duda wakati wa Ziara ya Mhe Mwakilishi Simai Mohammed Said na Naibu Waziri wa Ardhi Maji Mishati na Mazingira Mhe Juma Makungu Juma. ili kuondoa kero za Wananchi wa Jimbo hilo kwa upatikanaji wa Maji Safi na Salama. 
Katibu wa Kamati ya Maendeleo Dunga Ndg. ya Jimbo Khamis Haji Mkasaba akizungumza wakati wa ziara hiyo kutembelea vyanzo vya maji katika Jimbo hilo.  
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa ziara hiyo ilioazia katika kisima cha Maji cha Dunga kinachotowa huduma kwa wananchi wa Dunga na sehemu nyengine katika Jimbo hilo.
Msimamizi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA kituo cha Ubago Ndg Said Shaali, akitowa maelezo ya usambazaji wa maji katika kituo hicho kwa Wananchi wa eneo la Ubago wakati wa Ziara ya Mhe Naibu Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Mhe Juma Makungu Juma na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo hilo.ili kutatua kero za upatikanaji wa maji katika Jimbo lao.
Naibu Waziri wa Ardhi Maji Mazingira na Mishati Zanzibar Mhe Juma Makungu Juma akizungumza na Uongozi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakati wa Ziara ya Mbunge na Mwakilishi wa jimbo hilo kuangalia kero za upatikanaji wa Maji kwa Wananchi wa Jimbo lao jinsi ya kuzitatua kero hizo, wakiwa katika kituo cha kisima cha Ubago Wilaya ya Kati Unguja. wakiendelea na ziara yao.  
Diwani wa Wadi ya Dunga Mhe Ussi akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Mhe Juma Makungu, Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Halifa, bomba la maji linalopitiac shaji kwenda Dunga Kiembeni ambalo kwa karibu siku nyinge limekuwa likivujisha maji baada ya kupasuka. 
Naibu Waziri na Mwakilishi wakitembelea vyanzo vya maji katika eneo la Tunguu Jongo likiwa limechimbwa visiwa na Mradi wa Ras Al Haama katika eneo hilo ili kutowa huduma ya maji kwa wananchi wa wilaya hiyo











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.