Habari za Punde

Chama cha DP chaadhimisha mwaka mmoja tokea kufariki kwa Mchungaji Christopher Mtikila

ALI ISSA NA KIJAKAZI ABDLLA MAELEZO

Makamo Mwenyekiti Wa Chama Cha Dp Zanzibar Peter Agatano Magwira amesema wamepata pigo kubwa katika chama chao kwa kumpoteza alio kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mchungaji Christoper I Mtikila alio fariki kwa ajali ya gari mwaka uliopita

Amesema kiongozi huyo alikua muhimu kwao,kwachama,na familia yake jambo ambalo wataendelea kumkumbuka daima kwayale mema aliokitendea chama chao na hazina isio sahaulika.
hayo ameyasema leo huko Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa mila na utamaduni  wakati wa kumbumbu wa kifo cha mwenyekiti  huyo baada ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufa kwake.

Amesema chama kinamasikitiko makubwa kwa kuondokewa na kiongozi huyo hasa wakizingatia mchango wake aliokuwanao katika chama jambo ambalo kwao ni pengo na hawatarajia kupata kiongozi muadilifu na mchapakazi kama alivyo kuwa yeye.

“ Kwasasa hajatokea kiongozi kama yeye  kwani kiongozi alikuwa imara na hayumbishwi katika msimamo wa chama”alisema Magwira.

Aidha alisema serikali iwaweke wazi wananchi pindi  ikitokea tukio la kuuwawa  kwa viongozi  wa juu wa vyama vya siasa  ili kujua mwisho wa hatma ya watuhumiwa wa matukio hayo.

Makamo Mwenyekiti huyo akizungumzia mgogoro wa chama cha wananchi cuf alisema viongozi wa chama hicho wakae meza moja ili kuondosha mgogo wao kwani utapelekea pabaya chama chao na kupelekea kuja kufutwa kwa chama hicho

Aidha amesema kuwa msajili wa vyama vya siasa yupo kisheria na ana wajibu wa kuingilia migogoro wa chama chochote cha kisiasa kwa mujibu wa sheria,hivyo amewataka wananchi kumtambua kwa cheo chake.      Imetolewa Na Idara Ya Habari Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.