Habari za Punde

Jeshi la Polisi lawamani Pemba

Na Mwandishi wetu, Pemba

Wananchi wa shehia ya Chonga wilaya ya chakechake mkoa wa kusini Pemba wamelilalamikia jeshi la polisi kushindwa kuwadhibiti watuaji wa madawa ya kulevya katika maeneo yao hali inawafanya kujikuta wakiwa katika udhalilishwaji wa hali ya juu.

Wamesema kuwa katika shehia yao kumekua na ongezeko kubwa la vijana wanaotumia dawa za kulevya huku jitihada za wananchi na baadhi ya viongozi wa shehia hiyo zikigonga mwamba kwa jeshi la polisi katika mashirikiano ya kutatua kadhia hiyo.

Mmoja miongoni mwa wananchi katika shehia hiyo Halima Mabrouk Ali amesema kua,katika shehia hiyo hali ni mbaya nani yakutisha hasa kwa akina mama na watoto kutokana na vitisho na uhalifu unofanywa na baadhi ya vijana wanaotumia madawa ya kulevya shehiani kwao.

Amesema inapofika nyakati za saa 12 jioni kuelekea usiku hali huwa si shuari katika maeneo mengi ya shehia hiyo.

Nae Amina Juma Rajab mkaazi wa kipapo ameungana na wakaazi wengine kuzungumzia kadhia hiyo ambapo amesema vijana wengi katika shehia yao wameharibika kwa madawa ya kulevya.

Akizungumzia athari zitokanazo na vijana hao amesema, wahanga wakuu ni wanawake na watoto ambao mara nyingi hufikwa na udhalilishaji kiasi ambacho wanapokuwepo vijana hao mwanamke au mototo hawezi kupita maeneo hayo.

“Vijana hawa ni hatari sisi wanawake tunateseka maana wanakaa karibu na njia huwa hapapitikiti”alisema Amina.

Pia amesema suala la wizi wa mazao na majumbani umekithiri sana katika maeneo yao hali ambayo inawapashida katika maisha kijijini hapo.

Katika hali ya kuhuzunisha amesema kua vijana hao wanapopelekwa katika kituo cha polisi siku chakeche tu huwaona mitaani na kujinata na mambo yao na baadae kuendelea na vitendo viovu kama ilivyokua.

Hidaya Yussuf Salum katibu wa sheha wa shehia hiyo amesema shehia yao imeathirika sana na madawa ya kulevya kwa vijana kuanzia umri wa miaka 12 hadi 25.

Amesema ni kweli wanawake ndio wanaoteseka na vijana hao kiasi ambacho hata mtu awe mjamzito hawezi kuhudhuria vizuri clinik au akiwa msoamji wa kwenda  madarasani atashindwa kwa sababu vijana hao makaazi yao  ni maeneo ya njiani kunakopita watu.

Nae sheha wa shehia hiyo Bw:Yahya Husein Yussuf ameungana na wananchi wake kwakusema kua tatizo hilo lipo nani  kubwa shehiani mwake hali ambayo inawafanya washindwe kuishi kwa uhuru.
“wanawake kweli wanateseka na wizi umekithiri sana wa mazao na majumbani”alisema sheha huyo.

Amesema wamekua na mashirikiano mazuri na jeshi la polisi katika kadhia hiyo lakini wanavunjika moyo pale wanaona vijana waliyokamatwa siku chache tu wakiachiliwa na kurejea mitaani kuendeleza vitendo vyao.

“mashirikiano yapo mazuri siku nyengine utaona polisi wanavamia tu kuwakamata vijana hata mimi huwa sinataarifa ni vizuri sana lakini wakiwakamata siku mbili tatu wanaachiwa , kuna uzorotaji wa kuchukuliwa hatua, ukiuliza utaambiwa kesi haijakamilika upelelezi unaendelea kufanyika, sasa sisi tunasema mtu aliyekamatwa na madawa ya kulevya hadharani au amekamatwa na kuku hadhiri nnadhiri na mwenyewe akakiri kama kweli ameiba sasa sijui kunatakiwa ushahidi gani baada ya kuchukuliwa hatua, baadae anaachiwa tunaambiwa upelelezi bado unaendelea na anafanya kuliko yale na ukimuuliza anakwambia atafanya na hatuwezi kumfanya lolote”alisema sheha huyo.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba Kamishna msaidi mwandamizi Muhammed Shekhan Muhammed amesema kua, wananchi hawakueleza kitu cha msingi isipokua wameelza hivo ili kuona kama jeshi la polisi pengine litafokewa.

Amekiri kua chonga kuna tatizo kubwa la vijana kutumia dawa za kulevya hasa baghi na jeshi la polisi lilipambana mpaka kupiga risasi na hatimae walilisambaratisha genge la vijana hao.

Amesema katika tukio hilo waliwakamata vijana zaidi ya saba na mpaka sasa kuna kesi  IR 3/2016 ambayo mtuhumiwa Ali Sulum Khamis Busara (21) alikatamatwa na shurushi moja la Baghi na wengineyo na mpaka sasa vijana hao wapo mahakamani na kesi ipo kwa mkemia wa serikali kwa kipindi hiki kusubiri matokeo ili kesi ianze mahkamani.

Amesema wananchi wanaposema kua wanatoa taarifa nahazichukuliwi hatua amesema ni kinyume hatua wanazichukua, wanazisimamia na wahalifu wanawakamata.

Amesema hali ya Chonga hapo awali ilikua ni ya kutisha,kulikua magurupu ya hatari lakini  saivi kumetulia,wananchi wanapita na kufanya shuhuli zao kama kawaida na watuhumiwa waliyokamatwa na jeshi hilo  wanachukuliwa hatua kama sheria zinavyotaka.

Shehia ya Chonga ni moja kati ya maeneo yanayosemekana kukithiri kwa vitendo vya wizi na utovu wa vidhamu kwa vijana wengi kutokana na kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya kama vile mangi na unywaji wa pombe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.