Habari za Punde

Vijana waaswa kujiajiri kuliko kusubiri ajira serikalini

Na Salmin J Salmin

VIJANA katika kijiji cha shidi shehia ya Mkanyageni wilaya ya mkaoni mkoa wakusini Pemba,wametakiwa kujikita zaidi katika kufanyakazi kuliko kusubiria ajira kutoka kwa serikalini.

Hayo yameelezwa na Ndugu Abdaalla Khamis Ali alipokuwa kizungumza na mwandishi wa habari hizi  wakati alipokua akitembelea maeneo mbalimbali kujua changamoto zinazowakabili vijana ambapo alibahatika kufika nymbani kwa bwana Abdalla shidi mkoani Pemba.

Amsema kuwa baadhi ya vijana hatawataki kujiajiri wenyewe na badala yake  kusubiria ajira kutoka serikalini jambo ambalo hupelekea kujiingiza katika vikundi viovu kama vile matumizi ya dawa za kulevya, utapeli na ukabaji.

Kwaupande wake mjasiriamali Rashid Ali Faki amesema kuwa,vijna walio wengi hawataki kujishughulisha na kazi yoyote ile jambo ambalo huongeza ugumu wa maisha na kuwa mzigo mkubwa kwa familia zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.