Habari za Punde

Dk Shein: Toeni ushahidi mahakamani kumaliza udhalilishaji


Na Haji Nassor, Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed Shein, amewataka wananchi wasisite kutoa ushahidi makahamani, pale wanapotakiwa kufanya hivyo, ikiwa ni hatua moja wapo ya kupunguza matendo ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
DK Shein ameeleza hayoa jana, uwanja wa Tenis Chakechake baada ya kuzindua na kisha kulitembelea, jengo la Mahakama kuu Chakechake Pemba, na kusema wananchi wanayo nafasi kwa upande wao kumaliza kesi hizo.
Alisema suala la kupunguza kesi za udhalilishaji, lina wigo mpana ikiwemo la wananchi kwenda katika mahakama mbali mbali kutoa ushahidi, pale wanapotakiwa na waendesha mahitaka kufanya hivyo.
Alisema wapo wananchi wamekuwa wakipuuza suala la kutoa ushahidi mahakamani, kwa kuona wanasumbuliwa na kupotezewa muda wao, jambo  ambalo ni kinyume, maana hakuna kesi inayohukumiwa pasi na ushahidi.
Hivyo, amewasisitiza wananchi hao kutopuuza maagizo ya waendesha mashitaka, mahakama na majaji, na badalayake wapaniwe kutoa ushahidi mahakamani.
“Mimi niwaombe sana wananchi wetu, wasisite kutoa ushahidi mahakamani, ili majaji na mahakimu wetu, wapate kuendelea na kesi mbali mbali’’,alifafanua.
Katika hatua nyengine rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed Shein amewataka majaji na mahakimu hao, kutochelewesha utoaji wa haki kwenye mashauri yanayowasilishwa mahakamani.
Alisema wanapochelewa kutoa haki hiyo, wapo wananchi wanahisi kuchoshwa ya panda shuka na nenda rudi ya mahakamani, hivyo uharaka wao utasaidia wananchi kuwa na imani nao.
“Nanyi majaji na mahakimu wetu, fanye juhudi za makusudi ili kuhakikisha, mnafanya haraka kutoa haki, maana haki inayochelewesha ni haki iliokataliwa’’,alifafanua kwa kusisitiza kwa msemo.
Kwa upande mwengine Rais huyo wa Zanzibar, amesema ni imani yake sasa baada ya kumalizika kwa matengenezo makubwa ya jengo la Mahakama kuu Chakechake Pemba, sasa watendaji hao watafanya kazi zao kwa ufanisi.
Alieleza kuwa, sio tu majaji na mahakimu, lakini hata wapiga chapa, wahasibu, waendesha mashitaka na wengine wanaouhudhuria makahamani.
“Sasa naamini mtafanya kazi zenu kwa faragha tena ya kutosha, maana nimeonyeshwa ofisi mpaka za majaji, mahakama ya watoto wakati naitembelea, hii yote nifaraja kwangu’’, alifafanua.
Hata hivyo rais huyo wa Zanzibar, alisema baada ya mtangenezo hayo makubwa, sasa watendaji wa mahakama watafikia dira ya mahakama kuu waliojiwekea.
Kuhsu kisiwa cha Pemba, kutokuwa na jaji mkaazi wa mahakama kuu, alisema hilo linawezekana kwa sasa, hasa baada ya matengenezo ya jengo hilo.
Alisema majaji wakuu kuweko kisiwani Unguja na kwenda kisiweni Pemba kwa siku inachangamoto zake ambazo zinahitajika kuangalia upya na idara ya mahakama.
“Mfumo wa majaji kuweko Unguja na kwenda Pemba, lazima utazamwe upya, maana unachangia gharama sana katika uendeshaji wa kesi na kikwazo ya kumaliza mashauri kwa wakati’’,alifafanua.
Wakati huo huo, Rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, ametumia nafasi hiyo, kuwaonya wanaobeza viongozi kwamba sasa basi.
“Uchaguzi umemalizika na rais kwa mujibu wa katiba ameshapatikana, sasa weleo wao wanaobeza serikali na viongozi waliopo, maana hii ni serikali ya anaeitaka na asietaka lazima aitii’’,alifafanua.
Mapema akisoma risala ya matengenezo hayo Mrajisi wa Mahakama kuu Zanzibar Goerge Joseph Kazi, alisema matengenezo ya jengo hilo tokea kujengwa kwakwe mwaka 1920 halijawahi kufanyiwa matengenezo hadi mwaka huu.
Alisema sasa matengenezo hayo ambayo yaliambatana na ujenzi kwa baadhi ya maeneo, yametanua nafasi kuwa kuwepo chumba cha mahabusu, washika fedha na wahasibu kutenganishwa tofauti na kabla.
“Jengo hili limendoa ufinyu wa nafasi, maana sasa kuna ofisi za majaji na mahakimu mbali mbali, lakini  sasa hata mfumo wa maji taka na maji safi sambamba na vyoo, liko vyema’’, alifafanua.’
Alisema katika matengenezo na ujenzi wa jengo hilo la mahakama kuu Chakechake, shilingi zaidi ya milion 373 zilitumiwa  na kampuni ya ZECCON LTD kulifanyia mtengenezo, baada ya kushinda tenda na kufanya kazi hiyo.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aliipongeza serikali kwa kulifanyia mtengenezo makubwa jengo hilo ambalo lilikuw ahali mbaya.
Alisema hatua hiyo ni sehemu ya utelezaji wa Ilani ya CCM ya uchagzui ya mwaka 2015/2020 na kuiomba serikali iendelee na hilo, maana bado mahakama mbali mbali kama vile za Mkoani, Wete na Konde hali hairidhishi.
Naibu waziri wa Wizara ya nchi afisi ya rais Katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora Zanzibar Khamis Juma Maalim, amewataka wanafanyakazi hao, kulitunza jengo hilo ili lidumu kwa muda mrefu.

Jengo hilo la Mahakama kuu Chakechake ambalo lilijengwa miaka ya 1922, awali lilikuwa na choo kimoja kilichokuwa kikitumiwa na mahabusu, wafanyakazi ambapo sasa kuna vyoo vitatu na vyumba vyengine kwa ajili ya majaji wa mahakama kuu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.