MAAFISA Wadhamini Kutoka taasisi mbali mbali za
Serikali Kisiwani Pemba, wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, wakati alipokuwa akifungua Mkutano
huo huko nje kidogo ya Mji wa Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
WAKUU wa Wilaya kutoka Wilaya nne za Micheweni,
Chake Chake, Mkoani na Wete Kisiwani Pemba, wakifuatia kwa makini hutuba ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe;Mohamed Aboud Mohamed,
hayupo pichani wakati akifungua kikao cha kuwajengea uelewa viongozi kuhusiana
na mpango wa kunusuru kaya masikini Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA)
AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, Salum Ali Matta, akiwakaribisha wageni katika mkutano kuwajengea uelewa viongozi kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini Pemba, mkutano huo uliofanyika nje kidogo ya mji wa Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
MKURUGENZI Mtendaji wa TASAF Makao Mkuu, Ledislaus
Mwamanga akitoa maelezo ya jumla juu ya mpango wa kunusuru kaya masini
Tanzania, katika mkutano uliowashirikisha viongozi mbali mbali uliofanyika
Wesha nje kidogo na mji wa Chake Chake.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA)
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Ahmad
Kassim Haji, akizungumza katika mkutano uliowashirikisha Viongozi mbali mbali
wa Serikali, juu ya mpango wa kunusuru kaya masikini Pemba, uliofanyika nje
kidogo ya mji wa Chake Chake Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA)
MWENYEKITI wa Kamati tekelezaji ya Tasaf Pemba,
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe;Mwanajuma Majid Abdalla,
akizungumza neno katika mkutano wa kuwajengea uwelewa Viongozi juu ya mpanbgo
wa kunusuru kaya masikini Pemba, uliofanyika nje kidogo ya Mji wa Chake Chake
Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Mhe:Mohamed Aboud Mohamed akifungua mkutano maalumu wa kuwajengea
uelewa viongozi wa Serikali juu ya Mpango wa kunusuru kaya masikini Pemba,
uliofanyika nje kidogo wa mji wa Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman,
akitoa neno la shukurani baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhe:Mohammed Aboud Mohammed, kufungua mkutano maalumu wa kuwajengea uwelewa
Viongozi wa Serikali juu ya Mpango wa Kunusuru kaya masikini Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe:Mohammed Aboud Mohammed,
katikati wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano maalumu huko
Wesha nje kidogo ya mji wa Chake Chake.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA)
No comments:
Post a Comment