-Awataka wananchi kuendelea na
shughuli zao bila ya hofu
-Asema anaejua hatma yake sio mtu ni
Muumba
Na Haji Nassor, Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed Shein, amerejea kauli yake ya kuwataka
wananchi kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila ya hofu, maana
uchaguzi umeshamalizika na yeye ndie rais halali wa Zanzibar, na wala hakuna mahakama yoyote
duniani inayoweza kumng’oa.
Alisema
wanaokwenda mashariki na magharibi ya dunia waendelee kufanya hivyo, na hata
kuendelea kwenda kwenye mahakama ya kihalifu ya ICC, lakini amewahakikishia
wananchi kuwa, hakuna uchaguzi mwengine hadi mwaka 2020.
Dk:
Shein ameeleza hayo kwa nyakati tofauti, mkoa wa kaskazini Pemba, alipokuwa
akizungumza na wananchi wa wilaya ya Micheweni mara baada ya kutembelea ujenzi
wa ukumbi wa halmshauri na ufunguzi wa skuli ya Maandalizi Junguni Gando.
Alisema
yeye yupo madarakani kwa mujibu wa sheria na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,
na ameingia Ikulu baada ya wananchi kumpigia kura na kushinda kwa kishindo,
hivyo kama kuna yoyote hakuridhishwa na hilo, aende mahakamani.
Dk:
Shein amewataka wananchi hao wa Micheweni na Gando kuwapuuza wanaosema kuwa
uchaguzi utarejewa au kuwa yeye hamaliza muda wake wa miaka mitano ijayo, kwa
kisingizo cha kuwepo kwa mahakama ya kimataifa kumuondoa.
Rais
huyo wa Zanzibar, amekuwa akirejea kauli hiyo mara kwa mara, ambapo aliwataka
wananchi hao kuelewa kuwa, yeye ndie rais halali, na ameshawachagua mawaziri,
makatibu wakuu na watendaji wengine na sasa kilichopo mbele yake ni kutekeleza
Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Alisema
wapoa wanaopita pita na kuwaeleza wananchi kuwa rais wa Zanzibar hatomaliza
muda wake wa uongozi na wakisambaaza maeneno kuwa, ataondolewa na mahakama za
kimataifa.
Aliwaeleza
wananchi hao, kuwa waendelee kuwapuuza wale wanaoutafuta urais wa Zanzibar nje
nchi na hasa baada ya kushindwa kwa hiari zao, kuingia kwenye uchaguzi wa
marudio wa mwezi Machi mwaka huu.
“Wananchi
ondoeni hofu, mimi ndie rais wenu, milionichagua Machi 20, mwaka huu, na wala
hakuna mahakama wala mtu wa kuniondoa, na mwenye mamlaka ya kujua hatma ya umri
ni Allah pekee’’,alifafanua.
Akizungumzia
ukumbi huo wa Halmshauri ya Wilaya ya Micheweni, Dk: Shein amesema anaamini
utatanua wigo wa kiuchumi na mapato kwa halmshauri hiyo.
Alieleza
kuwa, ukumbi huo ambao ni wa kisasa, utatumiwa na hata wananchi wa kawaida, kwa
shughuli zao mbali mbali ikiwa ni pamoja mikutano na harusi.
‘Ukumbi
huu, nimeshaukagua na ni wakisasa, sasa hapa halmshauri itaongeza pato lake,
lakini na nyinyi wananchi mtaumia kwa shughuli zenu’’,alifafanua.
Wakati
huo huo rais huyo wa Zanzibar na Mwneyekiti wa baraza la Mapinduzi dk: Ali
Mohamed Shein wakati akiizindua skuli ya Maandalizi ya Junguni Jimbo la Gando,
amewataka wananchi kuwa karibu na watoto wao hasa wa maandalizi.
Alisema
sera ya elimu ya mwaka 2006, imekuwa ikiweka mkazo umuhimu wa elimu ya
maandalizi, maana hapo huandaliwa mwanafunzi kwa ajili ya elimu ya juu.
Katika
hatua nyengine rais huyo wa Zanzibar, alisema kabla ya mapinuzi ya Zanzibar ya
mwaka 1964, hakukuwa na mtoto wa kinyonge alikuwa na uwezo wa kusoma elimu ya
maandalizi, jambo ambalo kwa leo halipo.
“Azma
ya rais wa kwanza wa Zanzibar wa kutangaaza elimu bure, imetusaidia sana leo
hii, na ndio maana hata baada ya kuwepo kwa michango na sasa imeshafutwa kwa
lengo lilelile ili kila mtoto mwenye uwezo wa kusoma apate elimu’’,alifafanua.
Mapema
Katibu mkuu wizara ya nchi afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Abdalla
Joseph Meza, alisema hadi kukamilika kwa jengo hilo la skuli ya maandalizi
shilingi zaidi ya milioni 82 zilitumika, ikiwa nguvu za wananchi ni shilingi 11
na TASAF III ilichangia shilingi milioni 61.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, aliipongeza serikali kwa
juhudu zake za makusudi katika kuchapuza
maendeleo ya kielim siku hadi siku.
Akisoma
risala ya wanacnhi wa shehia Gando, mwalimu Mkuu wa skuli ya Gnado Mmaka Hamad Nassor, alisema baada ya kuona
watoto wao wanahangaika, walifikia uamuzi wa kuanza kujenga skuli hiyo yenye
madarasa matatu, na kisha TASAF III kuwaunga mkono.
Ujenzi
wa skuli hiyi ilioanza mwaka jana, litatakuwa na uwezo wa kusomewa na wanafunzi
100 kwa wakati mmoja, ambapo hadi sasa skuli hiyo ya maandalizi ina mwalimu
mmoja, huku rais wa Zanzibar akiiagiza wizara ya elimu kupeleka waalimu skulini
hapo.
No comments:
Post a Comment