Habari za Punde

Vitimbwi na adha nyumbani kwako mwenyewe

Na Mkaazi wa mji mkongwe

Vitimbwi vya nchi hii vingi. Leo hili kesho lile. Kesho kutwa ...Alimradi badala watu kukaa tukafanya kazi za maendeleo au kunyanyuana kutwa ni kufitiana au tunatafuta njia na sababu za kukomoana. 

Kweli hii nchi ya amani kama hivi ndivyo tunavyoishi? Asubuhi ya leo nimeamka na kukuta mtu au binaadamu (ingawa ana tabia zaidi ya mnyama asiye wa kufugwa) kaninyea choo cha kutosha sehemu kama 3 nje ya mlango wangu. Na si mara ya kwanza. 

Jana yake mtu kama yeye alikula kwenye baraza akanitapakazia chakula alichobakisha barazani hapo. Kama leo si uharo, kesho makamasi nk. Juzi nimemkuta mtu ananikojolea kwenye ukuta. 

Kumuuliza kaja anataka kunipiga jiwe kwangu mwenyewe kisa nimethubutu nini kumuuliza! Kwa nini nimemkataza? 

Ukizifuata mamlaka husika hakuna linalofanyika. Polisi watakutusi na kukupotezea muda. Mamlaka zinazosimamia masuala au ya usafi au mji mkongwe nk alimradi lalamiko halihusu hoteli ya kimataifa hata hawatasogea.

Suali langu, Mamlaka zinajali amani kwa wageni tu? Sisi wakaazi, wenyeji tuishi tu kwenye tension zisizokuwa na msingi.

 Ukitaka kufuatilia na kusimamia haki yako utaambulia kuvunjiwa heshima kudhalilishwa siku nyingine ufikiri mara mbili kwenda kusumbua wanopokea mishahara kwa kutuna katika viti vyao bila kutelekeza wajibu wao. 

Haya ndio maisha yetu siku nenda siku rudi! Kamwe barka haisogei nchi hii kama hatujiadabishi na kupenda kusimamia haki. Au kama tunakosa kuheshimiana. 

Hata tukirukuu na kusujudu mara 75! Alimradi roho haziko radhi zinaudhika na zinasononeka, hasada na dhulma zimetawala, abadan tusitaraji barka wala ustawi !

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.