Habari za Punde

Waziri Makamba afanya ziara Wilaya ya Kaskazini Pemba

 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea  mara baada ya kupokea taarifa  ya Mkoa wa  Kaskazini Pemba alipokua ziarani Mkoani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka Wananchi wa Zanzibar  kuulinda na kuuheshimu Muungano pamoja na mapinduzi tukufu ya Zanzibar. Ameyasema hayo alipokua ziarani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aliongeza kuwa anaipongeza Serikali ya Mkoa kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha  wanasimamia usalama kwa raia wote . Akiwasilisha  taarifa kwa Mh Waziri, Katibu tawala wa Mkoa wa Kasazini Pemba Mohamed Ali alitaja changamoto zinazowakabili ni uchakavu wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  hivyo kuomba Waziri awsaidie.

 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba yupo katika ziara mkoani Kaskazini Pemba pamoja na Unguja.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Yusuf Mohamed Ali akisoma taarifa ya Mkoa wakati akiiwasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba alipotembelea mkoa huo huko Pemba
 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  (aliyenyoosha mkono)  akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Wete- Pemba Bwana Rashid  Hadid Rashid wakati alipokua ziarani mkoani Kaskazini Pemba.
 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akikagua mazingira ya jengo ala Ikulu ndogo ya Ofisi ya Mh Makamu wa Rais lililopo Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia kingo za uzio wa  jengo la makazi ya  Makamu wa Rais huko Wete- Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.