Habari za Punde

Waziri Makamba atoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa mbunge wa Dimani - Hafidh Ali Tahir

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano Mazingira Mh. January Makamba akiwa pamoja na mjane wa Marehemu Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani Zanzibar(CCM) Bi. Shekha Said alipoenda kuwapa pole wanafamilia huko nyumbani kwa Marehemu Maungani Kisiwani Zanzibar. Mheshimiwa Waziri hakuwepo Nchini wakati msiba wa Mbunge huyo unatokea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwapa pole wanafamilia wa Marehemu Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani(CCM) alipowatembelea nyumbani kwa Mbunge huyo huko Maungani Zanzibar. aliyekaa kushoto ni ni baba mlezi wa Marehemu Mzee Kombo M. Kombo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwapa pole wanafamilia wa Marehemu Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani (CCM) alipowatembelea nyumbani kwa Mbunge huyo huko Maungani kisiwani Zanzibar. Aliyekaa wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Mh. Ayoub Muhammed Mahamoud.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.