Habari za Punde

Maandamano ya Zafa Kuadhimisha Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W)

Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW yakipita katika mitaa ya michezani kuelekea katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya maadhimisho hayo. Jumla ya Vyuo vya Quran 35 vimeshirika Zafa hiyo ya maandamono hayo na kupokelewa na Mgeni Rasmin Sheikh. Khamis Abdulhamid.
Watoto wakiwa wamepanda farasi kuashiria usafiri uliotomika wakati wa enzi za Mtume Muhammad  S.A.W, wakielekea katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar kuadhimisha siku hiyo. 
Viongozi wa Kamati ya Zafa Zanzibar wakiongoza maandamano hayo kuelekea katika viwanja vya mnazi mmoja ili kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W, yalioanzia katika viwanja vya Masjid Mushawar Muembeshauri na kumalizikia katika viwanja vya mpira mnazi mmoja Zanzibar. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.