Habari za Punde

Mchezo wa Mwisho wa Kombe la ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 Kati ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja na Kaskazini B Unguja Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu Kaskazini B Imeshinda kwa Penenti 5-4. na Kusonga Mbele Robo Fainali.

 
Viongozi wa Wilaya za Kaskazini Unguja wakifuatilia michuano hiyo wakasti zikicheza Timu zao na Wilaya katika michuano ya Kombe la ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 Kukuza vipata vya watoto katika Soka Zanzibar Michuano hiyo imeandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC). michuano hiyo inafanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.  
Kikosi cha Timu ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja kilichopambana na Timu ya Wilaya jirani Kaskazini B Unguja na kukubali kipigo kwa njia ya matuta na kuyaaga mashindano hayo hatua za mwazo.   
Kikosi cha Timu ya Wilaya ya Kaskazini B Unguja kilichotoka na ushindi kwa njia ya matuta dhidi ya Timu ya Kaskazini A Unguja baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo huo wa kuwania Kombe la ZBC Watoto Mapinduzi Cup U-17 mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.

 Wachezaji wa Timu ya Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakishangilia ushindi wao dhidi ya Wapinzania wao Wilaya ya Kaskazini A Unguja baada ya kuwashinda kwa mikwaju ya penenti 5-4.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.