Habari za Punde

Mchezo wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup Kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys Iliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Taifa ya Jangombe Imeshinda 1--0.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Omar Hassan King mgeni rasmin katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup. akiwa na kamisaa wa mchezo huo Issa Ahmada wakielekea kukagua Timu.. Wakati wa mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo inayofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.


Kikosi cha Timu ya Jangombe Boys kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi kilichokubali uteja kwa majirani zao Timu ya Taifa ya Jangimbe kwa kufungwa bao 1-0.
 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Jangombe Wakombozi wa Ngambo kilichoilaza Timu ya Jangombe Boys katika mchezo wake wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku huu na kushinda bao 1-0.


Kocha wa Timu ya Jangombe Boys King akifuatilia mchezo huo wa timu yake ikiwa nyuma kwa bao moja lililofungwa katika dakika ya 85 ya mchezo kipindi cha pili. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.