Habari za Punde

Nahodha wa Timu ya Zanzibar University Amwaga Machoni Uwanjani.

Na. Mwandishi Wetu.

Kazi kubwa iliyofanywa na nahodha wa kikosi cha chuo kikuu cha Zanzibar(ZU) Awadh Othman kwa kuifikisha timu yake fainali za mashindano ya vyuo vikuu Afrika Mashariki iligeuka kuwa kilio baada ya kushindwa kuunyakua ubingwa wa mashindano hayo.


Penalti aliyopiga kwenye pambano la nusu fainali dhidi ya bingwa mtetezi Ndejje iliifanya ZU kutinga fainali na kuchuana na Chuo cha Kampala majira ya saa 7:30 mchana.
Pambano hilo lilionekana kuwa na upinzani mkali ukizingatia kuwa bingwa mtetezi kutoka Uganda alishaaga huku Waganda wakielekeza macho yao kwa wasomo hao wa Kampala.

Kwa upande wa Watanzania ilikua ni ZU pekee waliosalia kwenye mashindano hayo kwa upande wa mpira wa miguu huku sumait ya Zanzibar, Mzumbe, UDOM na Ardhi kutoka Tanzania bara wakiaga mapema.
Dakika ya tisa Nabil Amour alianza kutikisa nyavu kwa kuiyandikia ZU bao la kuongoza, kabla ya Buga Moses kuisawazishia Kampala kwenye dakika ya 27.

Machofu ya michezo miwili ya muda wa karibu yalianza kuonekana kiwanjani kwa wachezaji wa ZU kutokana na kushindwa kupiga mipira ya mbali.

Dakika tisa kabla ya pambano kwenda mapumziko Mugulus Ibrahim aliipatia Kampala bao la ushindi kwenye dakika ya 36 na kuipa timu yake ubingwa.

Timu zote mbili za Zanzibar Sumait na ZU zinatarajiwa kuanza safari ya kurejea nyumbani saa kumi alfajiri ya leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.