Habari za Punde

ZLSC : Vikosi vya SMZ zingatieni haki za binadamu katika utendaji wenu


Na Salmin Juma , Pemba

Vikosi wa ulinzi vya serikali ya mapinduzi Zanzibr SMZ vimetakiwa kuzingatia haki za binaadamu wakati wanapotekeleza wajibu wao kinyume na hivyo wanaweza kujikuta katika mazingira yasio salama kisheria.

Kwa muda mrefu sasa Tanzania ni mwananchama wa umoja wa mataifa UN na imesaini mkabata  wa kulinda haki za binaadamu na miongoni mwa wadau wanaotakiwa kuzilinda haki hizo ni vikosi maalum vya  SMZ  ikiwamo kikosi cha kuzia magezo KMKM, Jeshi la kujenga uchumi JKU na wengineo.

Hayo yamebainishwa leo na mratibu wa kituo cha huduma za sheria,  Zanzibar Legal Servies Centre  ZLSC upande wa Pemba  Bi Fatma Khamis Hemed katika mafunzo maalum yaliyofanyika katika ukumbi wa kituo hicho chakechake Pemba juu ya kuviongezea taaluma  vikosi maalum vya SMZ ya kuona umuhimu wa kulinda haki za binaadamu.

Amesema miongoni mwa walalamikiwa juu ya wavunjaji wa haki hizo ni vikosi, hivyo amewataka kua makini na kuzielewa vizuri haki za binaadamu ili kuzilinda wanapokua katika majukumu yao.

Hemed  amesema, haki za binaadamu ni mambo yote ya msingi ambayo kama mwanaadamu anatakiwa ayapate, amesema kuna wataalamu wengine wamekwenda mbali zaidi ambapo wasema haki za binaadamu ni tokea mtoto akiwa tumboni na ndio maana kuna adhabu kwa wanao toa ujauzito.

Amesema katiba ya Zanzibar inatambuwa uwepo wa haki hizo na inasema kua watu wote ni sawa mbele ya sheria, hivyo amewataka wanavikosi hao  kuzilinda haki za binaadamu hata inapotokea wametakiwa kwenda kumkataba mtu, inatakiwa kufuata taratibu zinzozingatia haki hizo bila ya kutumia nguvu kupita kiasi iwapo anaetakiwa kukamatwa hakuonesha nia ovu yoyte.

Akiwasilisha mada ya haki za mtuhumiwa na mwanafunzi wa chuo cha mafunzo, afisa mipango wa  ZLSC Pemba Khalfan Amor Muhammed huku akiwaguza  kikosi cha askari mafunzo MF amesema kua, jeshi hilo ni la kutoa mafunzo ya amali kwa wanafunzi  ikiwamo kilimo, ufugaji, uchongaji na mengineyo.

Amesema kinachotakiwa mwanafunzi akitoka awe na ujuzi ili aweze kufanya kazi aliyojifunza chuoni "haitakiwi mwanafunzi kuteswa au kuvunjiwa haki zake kwasababu yeye bado ni mwanaadamu hivyo ana haki za msingizi zinazotakiwa kulindwa popote pale" alisema Muhammed

Haki za binaadamu ni pamoja na  haki ya kuishi, kula vizuri, elimu, kutodhalilishwa na kila kilichowajibu kwa mwanaadamu kukipata.

Mafunzo hayo ni ya siku mbili ambapo yataendelea tena kesho katika mada mbalimbali zitakazo toa elimu ya kutosha juu ya vikosi hivyo katika kuzingatia haki za binaadamu wakati wa utendaji wa kazi wao, ili kuhakikisha kila mtu nchini Zanzibar anaishi kwa amani na haki zake zinahifadhiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.