Habari za Punde

Wafanyabiashara waagizwa kuhifadhi kumbukumbu za biashara

Na Salmin Juma, Pemba
Afisa Uhusiano ZRB, Makame Khamns alipokuwa akizungumza na wafanyabiasharaWafanyabiashara visiwani Zanzibar wametakiwa kua na utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu katika biashara zao ili waweze kujua mwenendo mzima wa biashara pamoja na kuisaidia serikali katika kukusanya taarifa mbalimbali ambazo ni muhimu kwa wafanyabiashara na taifa kwa ujumla.

Inaonekana baadhi ya wafanyabiashara  wengi wao hawajui au kwa makusudi hawaweki kumbukumbu katika shughuli zao za kibiashara ikiwamo kutotoa risiti hali ambayo inayoifanya bodi ya mapato Zanzibar ZRB  kukosa baadhi ya makusanyo kwa  wafanyabiashara hao.

Akizungumza na wafanyabiashara hao juzi katika kikao cha kuimarisha mahusiano  baina ya ZRB na wafanyabiashara katika ukumbi wa hoteli ya Hifadhi Chakechake Pemba  afisa uhusiano wa ZRB  Makame Khamis Muhammed  amesema kua kutotoa risiti za mauzo kwa ni kosa kisheria hali ambayo inaweza kumfanya mfanyabiashara kuingia katika mkono wa sheria.

Amesema kwa wenye mahoteli na nyumba za kulalia  wageni ndio wengi miongoni mwao wasioweka kumbukumbu jambo ambalo hupelekea serikali kutojua ni aina gani ya wageni walioingia nchini na ni kwa kazi gani, hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuitika wito wa kutoa risiti kwa kila kunapohitajika kufanya hivyo.

Maafisa wa ZRB wameeleza kua mtu yeyete atakaekamatwa kwa kutotoa risiti adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano.

Nao wafanyabiashara hao kwa pamoja wameonyesha kukubalina katika hilo huku wakitoa wito kwa wenzao nchini kufuatasheria ili kujinusuru kujiweka katika hali mbaya kibiashara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.